MUSA LEONARD MDEDE akitoa neno katika kongamano la vijana wa katoliki
baadhi ya vijana wakimsikiza mdede katika kongamano hilo.
baadhi ya viongozi wa vijana hao wakiwa makini kumsikiliza mdede
mdede akiingia katika ukumbi uliokuwa unafanyika sherehe
na fredy mgunda, iringa
Vijana wa kikatoliki waliokuwa kwenye kongamano lililofanyika katika kijiji cha ulete wamewataka wananchi wa jimbo la kalenga kuelekeza macho na masikio yao kuhakikisha wanamchagua kijana
mwenzao ambaye ameonekana kuwa na uwezo wa kuwa kiongozi bora na kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.
Wakizungumza katika kongamano hilo vijana hao walisema kuwa hawajapata kuona kijana anayejiamini na kuonesha wazi mbinu za kulikomboa jimbo katika nyanja ya kimaendeleo.
“Jimbo la kalenga linawasomi wengi lakini jimbo hilo bado halina maendeleo ya kuridhisha licha ya kuwa na vitega uchumi vingi ambavyo vingeweza kuiongezea mapato na kukuza uchumi wa jimbo hilo,kwa mipango na mbinu ambazo mose madede amezionyesha zinatufaa kabisa wananchi wa jimbo la kalenga”. walisema vijana hao.
Lakini waliongeza kwa kuwataka vijana na wananchi wa jimbo la kalenga kutofanya makosa katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kumchagua kiongozi anayewafaa na kujiamini kwa kuwaletea maendeleo na kuwatetea wananchi wake.
Nao viongozi wa vikalia tosamaganga walimsifu kijina moses kwa kujiamina na kuwaonyenyesha vijana wenzao kwa maneno na ujumbe wa kuwapa njia muhimu za kufikia malengo yao katika maisha.
Waliongeza kwa kusema kuwa baadhi ya vijana waliokosa hutuba ya moses mdede wamekosa kitu cha muhimu sana lakini akawaomba vijana hao wakirudi nyumbani kwao basi wafikishe ujumbe kwa wananchi na vijana waliokosa kongamano hilo kwa kuwa wao ndio mabadiliko ya sasa.
“Vijana mbadilike msiwe kama vijana wa zamani nchi hii inahitaji viongozi wenye weledi wa kuwaongoza wananchi na kuwalete maendeleo mdede anafaa na anasifa zote za kuwa kiongozi kwa kuwa anasifa zote za kuwaongoza wanachi wa jimbo la kalenga hivyo wananchi msifanye makosa”.walisema viongozi hao.
Kwa upande wake sister kiliana sanga wa ulete alisema kuwa hajawahi kukutana na kijana mwenye uwezo mkubwa wa kifikra na mipango madhubuti ya kuleta maendeleo ya jimbo la kalenga.
Naye moses mdede aliwataka vijana kujitambua na kushemu maamuzi yao wakati wananfanya kitu sahihi kwa wakati sahihi kuwataka wasikubali kuchaguliwa kiongozi katika uchaguzi wa mwaka huu.
“Sasa ifike wakati vijana muwe na maamuzi ya kujichagulia viongozi sahihi vijana ni taifa la leo sio la kesho hivyo ukimchagua kiongozi kwa kununuliwa ujue kuwa atakapo ingia madarakani atawaongoza anavyowataka yeye na sio kuwaletea maendeleo kwa kuwa ameingia madarakani kwa kuwanunua”.alisema mdede
mdede aliwataka vijana kuacha kulalamika kila wakati na badala yake wafanye kazi kwa kujituma ili wajiletee maendeleo na kuacha tabia ya kufaata mkumbo katika kutafuta maisha bora.
“Viongozi wa dini nyie mnaka mara kwa mara na waumini wenu hiyo mnapaswa kuwapa elimu ya maisha na kuwajua viongozi wazuri kwa kuwa nyie mnakaramu hiyo,mfano leo hii mmekaa na vijana hao na kuwapa mafunzo mbalimbali hivyo mnapaswa kuwaambia ukweli juu ya mstakabadhi wa serikali yetu ambayo
imepoteza matumaini”.alisema mdede.
Lakini MDEDE aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuinua uchumi wa nchi.
MDEDE aliyasema katika kongamano la vijana wa katoliki katika kata ya ulete Iringa vijijini ambapo amewataka vijana kutambua umuhimu wao katika jamii ili kuleta madadiliko chanya kwa taifa .
Aidha, MUSA amesema kuwa wazee ni hazina kwa taifa kwa ushauri wa mambo mbali mbali ya kiuongozi lakini nguvu ya vijana inahitajika ili kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo na kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment