Mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya ya Iringa, Anjelika Kihakwi akibadilishana mawazo na kada mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa. Chadema walifanya mkutano wa hadhara jana katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia waliotangaza kugombea kubunge Jimbo la Kalenga.
Kada wa CHADEMA na Mwanasheria wa chama hicho, Lucas Sinkala Mwenda (kulia) ambaye ametangaza nia kugombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho amechukua fomu kwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Kalenga, Issa Nyamahanga jana katika Kijiji cha Ihomasa kata ya wasa Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa.
Mkazi wa Kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, Mzee Gaudencia Chogavanu Kikoti akiuliza swali kuhusu michango ya ujenzi wa maabara inayoendela kuwa ni mkubwa kulingana na hali zao za maisha kuwa duni, ambapo kila nyumba ina lazimika kutoa shilingi 30,000/- waktika wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana. Mkutano huo wa chama ulilengo kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia kwa wananchi Jimbo la Kalenga wilayani Iringa, mkoani Iringa.
Watia nia kugombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA, Mwanasheria wa chama hicho, Lucas Sinkala Mwenda (kushoto), Grace Tendega na Mussa Mdede wakiwasalimia wananchi wa Ihomasa, Kata ya Wasa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana. Mkutano huo cha walikuwa kwa lengo la kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia kwa wananchi.
Hatimaye kada wa Chadema
na mwanasheria msomi Lucas Sinkala Mwenda amechukuwa fomu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kugombea ubunge kwa mara ya pili kwenye kinyang’anyiro
cha uchaguzi mkuu wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Mwenda aliyekuwa mgombea kwenye
kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga ambaye aliyewashinda wagombea wengine 12 katika kura za maoni ndani ya
chama alipokwa ushindi na chama hicho na
kikamteua mshindi wa pili Grace Tendega
kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo.
Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe alimtaja mgombea huyo kuwa ni Grace Tendega. Mbowe alisema kuwa,
awali vyombo vya habari vilikuwa vimemtangaza Lucas Mwenda kuwa ndiye
atakayewania nafasi hiyo, jina ambalo halikuwa limepewa baraka na Kamati Kuu
yenye uamuzi wa mwisho.
Akifafanua zaidi, Mbowe
alisema kuwa ingawa Lucas Mwenda alipata kura 132, Kamati Kuu imempitisha Grace
Tendega aliyepata kura 122.
Akizungumzia sifa za
Mwenda, Mbowe alisema: “Bwana Sinkala (Mwenda) bado kijana mdogo, mwanasheria
wetu na tunahitaji kumkuza zaidi, basi vyombo vyote vimeshauri nafasi hii apewe
mama Tendega kwa sababu ana sifa za kutosha,” alisema Mbowe.
Mwenda amekabidhiwa fomu
hiyo jana na Katibu wa jimbo la Kalenga, Issa Nyamahanga wakati mkutano wa
hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa,
wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa.
Mkutano huo ulilenga
kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha baadhi ya watia nia kupitia wa chama
hicho akiwemo Grace Tendega, Mussa Mdede na Lucas Sinkala Mwenda ambao idadi
yao inafika jumla watangania wanne waliochukua fomu mpaka sasa.
CHADEMA katika uchaguzi wa
kujaza nafasi ya Ubunge jimbo la Kalenga-Iringa lililoachwa wazi na marehemu
Dk.William Mgimwa, waliojitokeza kugombea na kura zao ni hawa wafuatao, Zuberi
Mwachula – kura (0), Mch.Samwel Nyakunga - kura (2), Aidan Pungili - kura
(2),Daniel Luvanga - kura (1), Rehema Makoga - kura (4), Henri Kavina - kura
(9), Vitus Lawa - kura (12), Akbal Sanga -kura (21), Anicet Sambala - kura
(22), Dk.Evaristo Mtitu kura (32), Musa Mdede - kura (48), Grace Tendega - kura
(122),Lucas Sinkala Mwenda - kura (132).
No comments:
Post a Comment