Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Ushindani (FCC), Allan Mlulla akitoka hotuba yake jana wakati semina ya kuelimisha wadau kuhusu masuala ya ushindani, kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa (RAS), Wamoja Ayubu akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya kuelimisha wadau kuhusu masuala ya ushindani, kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia jana.
Washiriki wa semina ya kuelimisha wadau kuhusu masuala ya ushindani, kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia kwa kufuatilia kwa makini mada zillizokuwa zinatolewa. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA WA SIMBAYABLOG)
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Ushindani (FCC), Allan
Mlulla amesema vita dhidi ya bidhaa bandia ni vita dhidiya watu wenye uwezo
mkubwa wa kifedha, dhidi ya wahalifu ambao hawatakubali kirahisi kuachana na
biashara hiyo.
Mlulla alisema hayo jana wakati semina ya kuelimisha wadau
kuhusu masuala ya ushindani, kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia
iliyofanyika mkoani Iringa iliyoandaliwa na Tume ya Ushindani.
Wawezeshaji wengine waliofanyikisha semina hiyo kutoka tume
ni Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Ushindani Martha Kisyombe, Ofisa
Mwandamizi, Utetezi wa Ushindani Alex Mmbagana Ofisa Mwandamizi, Elimu kwa
Mlaji Frank Mdimi.
Alisema kuwa ili kufanikisha vita hii, kila mtu ashiriki kwa
kukataa kununua bidhaa bandia ambazo kivutio chakekikubwa ni urahisi wa bei.
“Usiweke rehani afya yako, maisha yako, utu wako, heshima
yako na wala mtu asichezee akili yako kwa kukubabaisha na bisahara ya bidhaa
bandia,” alisema.
Aidha, alisema kuwa kupambana na bidhaa bandia (feki) tume
imefanyikiwa kukamata makontana 268 yenye thamani Tshs. 229, 500,000/- kwa
mwaka wa fedha 2013/2014.
Pia tume imepokea maombikutokakwa wamiliki wa bidhaa au
wawakilishi wao (Brand owner), kuomba tume kufanya ukaguzi na kukamata bidhaa
badia katika maduka yanayohisi kuuza bidhaa hizo.
Hata hivyo, tume kwa kushirikiana na brand owner imefanya
uchunguzu wa maduka 58 katika jiji la Dar es Salaam na kufanyikiwa kukamata
badhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na simu aina ya Samsung, Nokia na Tecno, kompyuta
aina ya HPs, vipodozi aina ya LIPER, NIVEA, vifaa vya michezo kama vile SIMBA
Sports, pombe kali aina ya Konyagi pamoja na vifaa vya ujenzi na umeme.
Alielezea pia baadhi
ya madhara ya bidhaa bandia katika uchumi na jamii kuwa; ni kama ukwepaji wa
kodi kwa sababu watu wanaojihusisha bidhaa bandia ni wahalifu na mara nyingi
hawalipi kodi za serikali, mtengezaji wa bidhaa bandia hawajibiki kwa athari
zinazoweza kumsibu mlaji, bidhaa bandia zinaleta madahra kwa mlaji kwa mfano
kifo, huondowa sokoni mwenye bidhaa halisi na hufukuza wawekezaji.
Hata hivyo, alisema kuwa walaji wengi nchini hawana weledi
katika masualaya kumlinda mlaji na kuongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika
kutoka kwa wadau wote kusambazaelimuna masuala ya mlaji,ili waona
hajayakuchukua hatua ya kutetea haki zao kwa manufaa yao na taifa.
Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa (RAS), Wamoja Ayubu wakati
akifungua semina aliwataka wafanyabiashara kuchukuwa jukumu la kuelewa kuwa
biashara ya bidhaa bandia ina athari kubwa kwa wananchi wenzetu na hivyo
tujihadhari na bidhaa bandia.
Rai yangu, “semina hii iwe hatua muhimu katika kutatua kero
za msingi za wananchi kwa kuwa inawafungua macho wadau mbalimbali wa biashara
kubaini sheria za ushindani, utetezi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia;
kubaini vyanzo na ukubwa wa changamoto na matatizo yaliyopo katika mfumo wa
uchumi wa soko na nyenzo zilizopo katika kukabiliana nayo.”
Aliwataka pia washiriki kutumia semina hiyo kujifunza mikakati
ya kupambana na bidhaa bandia nchini na kuwa mabalozi wazuri kwa
wafanyabiashara wenzao watakaporudi katika shughuli zao.
Alisema kuwa usimamizi wa uchumi wa soko ambao hufanyika
Tanzania na Duniani kote unalenga
kusimamia misingi ya ushindani na kuhakikisha kuwa matarajio ya mizani sawa
yanapatikana.
Tume ya Ushindani ni chombo kinachosimamia utendaji wa uchumi
wa soko kwa nia ya kuhakikisha kuwa misingi ya ushindani inalindwa na
kusimamiwa ipasavyo ili kuhakikisha kunakuwa na fursa sawa katika shughuli za
uchumi miongoni mwa wazalishaji, wasambazaji na walaji ambao ni watumiaji wa
mwisho wa bidhaa na huduma mbalimbali.
Tume imeundwa na Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 kwa
madhumuni ya kulinda na kutetea ushindani wa haki katika uchumi wa soko,
kumlinda mlaji dhidi ya mienendo onevu na potofu katika soko na shughuli
zinazoshabihiana na hizo.
Pia kwa Mujibu wa Sheria ya Alama za Bidhaa ya Mwaka 1963,
ambayo imefanyiwa marekebisho mbalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani
pia ana wadhifa wa Mkaguzi Mkuu wa Sheria ya Alama za Bidhaa (Merchandise Marks
Act), ambayo inaongoza mapambano dhidi ya bidhaa bandia.
No comments:
Post a Comment