Friday, 26 June 2015

UKOO WA CHIFU MKWAWA WAJITOSA UBUNGE JIMBO LA KALENGA...!

Lucas Sinkala  Mwenda: Ilivyokuwa wakati wa kura za maoni ndani ya Chadema wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga (Picha na Maktaba)

Mtia nia Mwanahamisi Semuyinga (Samahani ubora wa picha upo chini ya kiwango)

Kushoto ni Lucas Sinkala Mwenda, Grace Tendega na Mussa Mdede.

MTIA nia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika nafasi ya ubunge Jimbo la Kalenga, Mwanahamisi Semuyinga amerudisha fomu jana na kuwaomba vijana na kina mama kusonga mbele na vyama vya upinzani katika Uchuguzi Mkuu mwaka huu.

Mgombea huyu alitoa rai hiyo jana wakati akirudisha fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la kalenga katika ofisi za chama hicho zilizopo makorongoni, mjini Iringa.

Wagombea wengine waliochukua fomu na kurudisha ni pamoja na mwanasheria wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini Lucas Sinkala Mwenda, katibu wa Bawacha taifa, Grace Tendega na Musa Mdede.

Mtaalam wa kilimo huyo alisema kuwa ni wakati sasa wa vijana kuchagua mabadiliko.

Alisema ameamua kugombea ubunge kupitia Chadema kwa sababu chama hicho kimeshika hatamu katika mkoa wa iringa kuanzia iringa mjini na maeneo mbalimbali.

Mwanahamisi ambaye ametoka katika ukoo wakina chifu mkwawa alisema kuwa aliwahi kugombea ubunge katika jimbo la kalenga hilo kupitia chama cha wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu mwaka 2000.

Alisema kuwa ameamua kugombea ubunge katika jimbo hilo ili kutaka kuvaa viatu vya adam sappi mkwawa spika wa kwanza bunge la Tanzania baada ya kuona historia ya chifu mkwawa inapotea bila kuweka mazingira mazuri ya makumbusho la fuvu la mkwawa.

Alisema kuwa jimbo la kalenga linakabiliwa na changamoto nyingi na viongozi wote waliopita katika jimbo hilo hawajaweza kutatua matatizo ya wananchi.

Alisema kuwa endapo atateuliwa na chama chake kupeperusha bendera ya chama chake na kushinda uchaguzi mkuu, atahakikisha zahanati na shule za msingi zinajengwa.

“Jimbo la Kalenga halina zahanati za kutosha, halina shule za msingi za kutosha kunakopelekea wanafunzi wengi kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni,” alisema mtia nia huyo.

Wakati huohuo, kada wa Chadema na mwanasheria msomi Lucas Sinkala Mwenda arudisha fomu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kugombea ubunge kwa mara ya pili kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa. 

Mwenda aliyekuwa mgombea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Kalenga ambaye aliyewashinda wagombea wengine 12 katika kura za maoni ndani ya chama alipopokwa ushindi na Kamati Kuu na kumteua Grace Tendega kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaja mgombea huyo kuwa ni Grace Tendega. Mbowe alisema kuwa, awali vyombo vya habari vilikuwa vimemtangaza Lucas Sinkala Mwenda kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo, jina ambalo halikuwa limepewa baraka na Kamati Kuu yenye uamuzi wa mwisho.

Akifafanua zaidi, Mbowe alisema kuwa ingawa Lucas Mwenda alipata kura 132, Kamati Kuu imempitisha Grace Tendega aliyepata kura 122.

Akizungumzia sifa za Mwenda, Mbowe alisema: “Bwana Sinkala (Mwenda) bado kijana mdogo, mwanasheria wetu na tunahitaji kumkuza zaidi, basi vyombo vyote vimeshauri nafasi hii apewe mama Tendega kwa sababu ana sifa za kutosha,” alisema Mbowe.

Alifafanua kuwa uchaguzi uliofanyika Iringa ulikuwa ni sehemu tu ya vigezo vinavyotumiwa na chama kumpata mgombea mwenye sifa na ushawishi kwa wanachama wake.

Mwenda amekabidhi fomu hiyo jana kwa Katibu wa Jimbo la Kalenga, Issa Nyamahanga ambapo awali alichukua fomu hiyo wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa.

Mkutano huo ulilenga kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha baadhi ya watia nia kupitia chama hicho akiwemo Grace Tendega, Mussa Mdede na Lucas Sinkala Mwenda ambao idadi yao inafika jumla watangania wanne waliochukua fomu mpaka sasa.

Chadema katika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Ubunge jimbo la Kalenga-Iringa lililoachwa wazi na marehemu Dk.William Mgimwa, waliojitokeza kugombea na kura zao ni hawa wafuatao, Zuberi Mwachula – kura (0), Mch. Samwel Nyakunga - kura (2), Aidan Pungili - kura (2), Daniel Luvanga - kura (1), Rehema Makoga - kura (4), Henri Kavina - kura (9), Vitus Lawa - kura (12), Akbal Sanga -kura (21), Anicet Sambala - kura (22), Dk. Evaristo Mtitu kura (32), Musa Mdede - kura (48), Grace Tendega - kura (122),Lucas Sinkala Mwenda - kura (132).

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...