Saturday, 11 July 2015

MGOMBEA WA URAIS KUPITIA CCM KUJULIKANA LEO MJINI DODOMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti mjini Dodoma.

"Leo tarehe 7 mwezi wa saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-20 20 lakini pia utateua mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, ratiba ya vikao, leo tarehe 7 kuanzia saa tano tutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, sekretarieti hiyo ina ajenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya mkutano mkuu, ina ajenda kubwa ya kupitia maandalizi ya mkutano mkuu na kuthibitisha yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makablasha mbalimbali na maandalizi ya document mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo.


Kesho tarehe 8 kunategemewa kufanyika kikao cha kamati ya usalama na maadili cha chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.


Tarehe 9 kichama kutakuwa na shughuli kuu mbili ya kwanza asubuhi, kutafanyika uzinduzi au ufunguzi wa ukumbi mpya wa chama cha mapinduzi na ofisi zake ambao upo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma bila shaka baadhi yenu mtakuwa mmeona, mwenyekiti wa chama Rais Kikwete alipokwenda kutembelea kwahiyo ufunguzi wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi kabla mheshimiwa rais hajaenda kuvunja bunge, kama ratiba itabadilika tutawaambia lakini tarehe 9 tunahiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea mkutano mkuu.


Tarehe 10 tunategemea kuwa na kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi ambacho kikao hichi kitafanya mambo makubwa matatu ambacho kitafanya, kwanza kitateuwa jina la mgombea urais kwa upande wa Tanzania zanzibar, halmashauri kuu ya taifa kwa mujibu wa katiba ndio inayoteua jina la mgombea urais wa Zanzibar kwahiyo hiyo itakuwa ni kazi mojawapo itakayofanywa na Halmashauri kuu ya Taifa na kazi ya pili, watapitia pia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo itakayotumika kuombea kura na ndio itakayotumika kwa kipindi cha 2015-2020, na kutoka kwao hiyo ilani itapelekwa katika mkutano mkuu kwaajili ya kuhitimishwa.

Kazi ya tatu, halmashauri kuu hii itapokea majina matano kutoka kamati kuu ambayo yatakuwa yameteuliwa na kamati kuu, tarehe 9 na hapo watafanya kazi ya kupiga kura kupata majina matatu ya wanachama wa CCM walioomba kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Majina matano haya yatapigiwa kura kupata matatu na tarehe 11 ndio siku ya mkutano mkuu wa Taifa wa chama cha mapinduzi ambao una kazi kubwa mbili, moja ni kupitisha hiyo ilani ambayo itakuwa imepitishwa na halmashauri kuu ya Taifa na maandalizi ya ilani hiyo yamekamilika, tuliunda timu kama mnakumbuka tumewahi kuitangaza ipo chini ya Wasira imefanya kazi nzuri ya kutengeneza ilani nadhani safari hii tutakuwa na ilani nzuri sana ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote zilizopita lakini pia itatupeleka sasa kwenye hatua kubwa zaidi ya maendeleo ya nchi yetu.

Kazi ya pili, ni kupiga kura katika majina matatu yatakayowasilishwa katika mkutano mkuu ili kupata jina moja la mwanachama wa CCM ambaye ndiye atakuwa mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi, hivyo tarehe 11, itakuwa ni siku ya mkutano mkuu na mkutano mkuu huu utakuwa wa siku moja,lakini mkutano mkuu huu utaoneshwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, tv zote zitaonesha kuanzia ufunguzi ratiba ile mpaka wakati fulani halafu baadaye wakati wa matokeo na ufungaji wa mkutano karibia masaa sita au saba hivi tutauonesha moja kwa moja.


Ninachotaka tu ni kuwathibitishia watanzania tumejipanga vizuri chama chetu tupo wamoja tunaamini tutamaliza vikao hivi salama, na tutatoka tukiwa na ushindi, tutatoka tukiwa na nguvu, tutatoka tukiwa wamoja na bila shaka vikao hivi vitajenga msingi wa kushinda uchaguzi kwa kishindo sana mwaka huu.


Nataka pia nichukue nafasi hii kuwathibitishia wajumbe wa vikao vyote kuwa maandalizi yao yamekamilika na tunawatakia safari njema kutoka wanapotoka katika nchi yetu, tunawatakia afya njema na vikao vyema vya kamati ya maandalizi na tunawakaribisha sana Dodoma karibuni tukijenge chama chetu na demokrasia ya nchi yetu tuendelee kuimarisha demokrasia ya nchi yetu".

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...