WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku akiahidi kuendeleza safari yake ya matumaini iliyopigwa STOP na alivyoviita vikao vya Chama cha Mapinduzi (CCM) vilivyokiuka katiba yake.
Katika hafla rasmi ya kukabidhiwa kadi yake, iliyofanyika hii leo jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema mchakato mzima wa kumpata mgombea urais kupitia CCM uligubikwa na hila, chuki, majungu na uzushi dhidi yake.
Lowassa alisema maamuzi yaliyofanywa na vikao vilivyochuja jina lake na ya wengine, hayajawahi kufanywa katika historia ya chama hicho..
Alisema Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho ilipokonya madaraka ya Kamati Kuu na akakifananisha kitendo hicho na lugha ya mtaani ya kubaka demokrasia.
Alisema CCM ile aliyoiona Dodoma sio ile iliyomlea na kumkuza na akaomba watanzania wajiunge na kuing'oa madarakani
Alisema kama ilivyowahi kusemwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwamba CCM sio baba yangu wala mama yangu; “na mimi hii leo natangaza rasmi kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema. CCM sio mama yangu wala baba yangu. Naondoka CCM najiunga Chadema.”
Akizungumzia kashafa ya Richmond, Lowassa alisema ameitolea majibu mara kwa mara lakini watu wanataka kuziba masikio.
Lowasa alisema hausiki na kashfa hiyo na madai yanayotolewa dhidi yake kama yana ushahidi, mwenye ushahidi huo aende mahakamani.
MBOWE
SIASA ni mchezo ambao wakati mwingine gia ni lazima ibadilishiwe angani na kwamba chama ambacho hakiamini mabadiliko hicho sio chama.
No comments:
Post a Comment