Mkutano Mkuu wa Chadema kwa pamoja umempitisha Mwanasiasa Edward Lowassa kama mgombea Urais na Juma Haji Duni kuwa mgombea Mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 oktoba 2015.
Katika upigaji kura Kanda zote zimepiga kura ya NDIYO kwa Mh. Edward Lowassa na hakuna kanda iliyosema HAPANA, huku wakishangilia kwa nguvu.
Kanda ya Kaskazini, Kanda ya kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kusini na nyingine zote pia zimepiga kura ya NDIYO kwa Juma Haji Duni kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi nkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Akishukuru kwa uteuzi huo, Lowassa amesema; “nataka nichukue fursa hii kuwapongeza wenzangu waliojiunga name, maamuzi magumu lazima yafanyike.”
Alisema watanzania katika muungano huo wanatakiwa kujua kwamba wana nguvu kubwa, nguvu ya kuweza kuchukua dola asubuhi Oktoba 25.
“Nataka niwahidi kuwa nitapita kila jimbo la nchi hii, kwahiyo unapoondoka hapa kajiandae katika jimbo lako,” alisema.
Alisema katika mahojiano yake fulani na wanahabari aliwahi kuwaambia kwamba hana msamiati wa kushindwa.
Kufuatia matokeo hayo Mwanasiasa Edward Lowassa atapambana na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na wagombea wengine akiwemo Mchungaji Christopher Mtikila wa chama cha DP aliyechukua fomu ya urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment