Monday, 31 August 2015

LOWASSA ASAKA KURA IRINGA BAADA YA UZINDUZI WA KISHINDO DAR


Bibi kizee akiwa amejifunga skafu yenye maneno “Mabadiliko” wakati mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, akiwakilisha vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, Mh. Edward Lowassa, al;ipohutubia mkutano wa kampeni mjini Iringa leo Jumapili Agosti 30, 2015. Huu ni mkutano wa kwanza tangu azindue kampeni Agosti 29, 2015 pale Jangwani ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria

Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, akimnadi Mh. Lowassa mjini Iringa leo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Joseph Mungai, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015

Umati wa watu mjini Iringa kwenye mkutano wa kampeni wa UKAWA uliohutubiwa na Mh. Lowassa


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015
Mh. Lowassa akihutubia wananchi kwenye mkutanoi wa kampeni mjini Iringa leo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsalimia kijana mwenye ulemavu (jina lake hakupatikana kwa haraka) aliyehudhulia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Iringa Mjini, leo Agosti 30, 2015

Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa

Umati wa wakazi wa Iringa wakishangilia kwenye mkutano huo wa kampeni. (Picha zote na Othman Michuzi)

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...