Mwanahamisi Muyinga
Iringa. Makada wa Wawili wa Chadema Mbunge viti maalumu anayemaliza muda wake Chuki Abwao na aliyekuwa mmoja wa watia nia Jimbo la Kalenga aliyeshindwa kwenye kura za maoni wameibuka kidedea kwenye kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama cha ACT Wazalendo.
Makada hao waliibuka washindi kwenye uchaguzi uliofanyika juzi Chuki Abwao akishinda jimbo la Iringa mjini na Mwanahamisi Jimbo la Kalenga.
Makada hao sasa wanasubiri vikao vya juu vya chama ili kuidininisha kuwania ubunge na ikiwa vikao hivyo vitabiri Chuki atapambana na Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake Mchungaji Peter Msigwa, Mgombea ubunge kupitia CCM anayesubiri vikao vya juu vya chama hicho Frederick Mwakalebela na wagombei wa vyama vingine ikiwa watajitokeza.
Wakati Chuki akitarajia kupambana na wagombea hao Mwanahamisi anatarajia kupambana na Mbunge wa sasa anayemaliza muda wake Godfrey Mgimwa ambaye pia ni mshindi wa kura za maoni na kada mmoja kati ya Lucas Mwenda na Mussa Mdede wote kutoa Chadema ambao walipata kura 64 kila mmoja.
Katika uchaguzi uliofanyika kwenye ofisi za ACT Wazalendo Mkoa wa Iringa Chuki aliwashinda washindani wake Daud Masasi na Dk Ben Kapwani kwa baada ya kupata kura 23 akimuacha Masasi kwa kura mbili baad aya kupata kura 21 huku Dk Kapwani aliyetangaza kujitoa akipata kura tatu.
Katika uchaguzi uliofanyika kwenye eneo la Kihodombi kata ya Mlandege Mwanahamisi aliibuka mshindi kwa akupata kura 10 akifuatiwa na Daniel Mwangili aliyepata kura 7 huku Edward Mtakimwa na Kiduo Mgunga wakipata kura 3 kila mmoja.
Hata hivyo madai hayo yalipingwa na Mwenyekiti uchaguzi Mjini Iringa Placid Kamonga aliyesema uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi na demokrasia ya kweli kwa kuwa kura zilipigwa na kuhesabiwa kwa uwazi.
Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Iringa Kapwani alisema ni vema Masasi akasaini matokeo na kuendelea na mchakato wake kupinga matokeo ambao kwa mujibu wa waraka wa chama hicho mtu anayepinga matokeo atatakiwa kufanya kuwasilisha malalamiko yake ndani ya siku saba tangu kufanyika kwa uchaguzi.
Kwa upande wake Chuki ambaye alishinda uchaguzi huo aliwashukuru wapiga kura kwa akumuaamini na kueleza kuwa atahakikisha anafanya kazi ya kukijenga chama hicho kichanga kinachoingia katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza tangu kusajiliwa kwake.
Naye Mwanahamsi aliwashukuru wapigakura kwa kumuamini na kufafanua kuwa atahakiksha anatumia taalamu yake ya kilimo kuinua maisha ya wakazi wa Kalenga.
Katibu wa chama hicho Mkoa wa Iringa Aram Mbilinyi aliwataka makada wote wa ACT Wazalendo kuungana pamoja kushirikiana na aliyeshinda ili kutafuta ushindi kwenye uchaguzi kwa kuwa ushindi wa matokeo yaliyotokana na kura za maoni na y a watu wote.
“Hapa hakuna mshindi sisi sote tumeshinda wito wangu kwenu tuungane pamoja kuhakikisha tunawaunga mkono hawa mama zetu katika kipindi chote cha kampeni tukiwa na imani kuwa wakishinda wao tumeshinda sote”alisema Mbilinyi.
No comments:
Post a Comment