Thursday, 17 September 2015

CCM WAPANIA KULIGOMBOA JIMBO LA IRINGA MJINI


Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (Picha na Maktaba)


KIU ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukomboa Jimbo la Iringa Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, inazidi kuongezeka baada ya mgombea udiwani wa CCM kata ya kihesa kuwataka wananchi kutomchagua mbunge aliyemaliza muda wake kupitia chama cha demokrasia na maendelo (Chadema) Mch. Peter Msigwa kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake.

Mgombea huyo wa ata ya Kihesa, Kenani Kihongosi Laban alitoa rai katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Kihesa uliyofanyika viwanja vya kihesa sokoni jana.

Alisema kuwa mbunge huyo anayemaliza muda wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) aliahidi kujenga soko la kisasa la kihesa lakini hadi miaka mitano inakwisha soko hilo halijajengwa.

Aliomba wakazi wa kihesa wamchague katika uchaguzi mkuu wa 2015 iliakafanishe ujenzi wa soko hilo pamoja na mambo mengine ikiwemo masuala ya afya na elimu.

Alisema kuwa watangulizi wake waliopita hawajatekeleza ahadi walizoahidi lakini ni wakati kwa wananchi wa kata ya kihesa kumtuma yeye akatekeleze majukumu yao.

Kuhusu baadhi ya wananchi waliojenga milimani hususani eneo la mafifi mgombea huyo alisema akichaguliwa atakwenda kuwatetea ili wasibomolewe nyumba zao na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Aliongeza kuwa ili kufanisha azima hiyo aliwaomba wananchi wamchague kusimamia kata hiyo pamoja nakumchagua mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Frederick mwakalebela na mgombea urais kupitia chama hico Dkt John pombe magufuli ifikapo tarehe 25 oktoba mwaka huu.

Kenani Kihongosi aliwahi kuwa Katibu wa TAHALISO na  Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa avitaja vipaumbele vyake ambavyo atakwenda kusimamia atakapochaguliwa kuwa diwani ni pamojana afya na elimu.

Mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama akiwemo katibu wa ccm mkoa wa iringa Hassan Mtenga pamoja na mwenyekiti wa wilaya ya Kilolo Seth Mwamoto.

Kwa upande wake, katibu wa ccm mkoa wa iringa Hassan mtenga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa moja ya ahadi ya CCM ni kuipandisha timu ya lipuli iliweze kuipandisha hadhi kutokana mbunge aliyemaliza muda wake kuitelekeza timu hiyo.

Alisema katika pitapita yake amegundua kuwa vijana wengi wanapenda michezo na kuwataka wananchi wa jimbo la iringa mijini kuchagua mgombea wa CCM Frederick Mwakalebela ili aweze kutimiza azma hiyo.

Alisema kuwa anauhakika kuwa mgombea urais Dkt John Pombe Magufuli atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu kwa sababu amefanikiwa kutembea vijiji zaidi ya 1,885 tangu kuanza kwa kampeni wakati mgombea urais kupitia UKAWA mpaka sasa ametembelea zaidi ya vijiji 420.

CCM ililipoteza jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 baada ya kuchukuliwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayemaliza muda wake.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...