Wednesday, 30 September 2015

KONGAMANO LA KWANZA KWA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI IRINGA

Washiriki mbalimbali wa Kongamano la kwanza kwa wanawake masokoni-Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala msaidizi sehemu ya mipango na uratibu, Nuhu Mwasumilwe (katikati mbele walioketi mwenye kaunda suti)  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza, lililoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kupitia mradi Sauti ya Mwanamke Sokoni.(Picha na Friday Simbaya)




Baadhi wa washiriki wa kongamano la kwanza kwa wanawake wafanyabiashara masokoni wakiwa katika vikundi kujadili masuala muhuimu yanayohusu biashara na wafanyabiashara na kupanga njia zinazoweza kuwainua toka walipo.

Mwanasheria wa Equality for Growth, Hussein Sengu (kulia ) atoa semina juu ya haki za binadamu kwa sekta isiyo rasmi kwa wanawake wafanyabiashara sokoni katika Manispaa ya Iringa jana.


Baadhi wa washiriki wa kongamano la kwanza kwa wanawake wafanyabiashara masokoni wakifuatilia kongamano kwa makini.


Afisa Mradi wa Equality for Growth (EfG), Susan Sitta akimkadhi zawadi mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala msaidizi sehemu ya mipango na uratibu, Nuhu Mwasumilwe baada ya kufungua kongamano la kwanza kwanawake wafanyabishara masokoni Tanzania kupitia Mradi wa 'Sauti ya Mwanamke Sokoni' jana. 



Afisa Mradi wa Equality for Growth (EfG), Susan Sitta alisema kuwa EfG ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kuinua nafasi ya wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi. 

Wanawake walioajiriwa au kujiajiri katika sekta isiyorasmi ni walengwa wakuu na wadau wa shirika hili. 

EfG inajenga uwezo wa wanawake hawa kutambua fursa juu ya masuala yanayohusu maisha yao. 

Ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa kwa kundi hili EfG inaamini ushirikishwaji na ushiriki wa wanawake na wanaume kwa pamoja utapelekea kuwepo kwa maendeleo endelevu.

Alisema kuwa kongamano hilo yenye kauli mbiu "Kujenga mshikamano wa wanawake katika sekta isiyo rasmi Tanzania" lilikuwa na malengo ya kujadili masuala muhuimu yanayohusu biashara na wafanyabiashara na kupanga njia zinazoweza kuwainua toka walipo.

Na lengo lingine ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kwa lengo la kujenga mshikamano.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...