Taasisi ya Tanzania Development Initiative (TADIP) itakutana na waandishi wa habari Hotel ya Regency, Mikocheni, Dar es Salaam, leo saa 10.30 jioni kwa ajili ya kutoa matokeo ya utafiti wa kura ya maoni kuhusu Uchaguzi Mkuu.
Ngoja tuwasikilize na hawa kuwa watazungumza nini juu ya uchaguzi Mkuu.
======================
Kinachoendelea hapa Regency Hoteli muda huu ni George Shembusho Mkurugenzi wa Bodi ya TADIP, anazungumza na waandishi wa habari anasema walifanya mchakato wa utafiti kutokana na mahitaji na mazingira kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
-TADIP ilifanya utafiti mwezi wa 5 na wa 6, anasema matokeo yaliharibika kutokana na mambo kuingiliana na bodi ya ukurugenzi iliukemea kutokana na baadhi ya watu kuuchukua na kuuchapisha kwenye gazeti Agosti 4.
-Anasema katika siku za karibuni kumetokea kasumba ya umma kutafsiri utafiti unaotolewa siku za hivi karibuni kwa njia tofauti kutokana na mazingira jinsi yalivyo.
Kushoto ni Kostastin Deus,Mtafiti Mwelekezi akiwa na George Shembusho Mkurugenzi wa Bodi ya TADIP
Anamkaribisha Kostastin Deus, Mtafiti Mwelekezi kueleza jinsi walivyofanya hadi kupata matokeo ya utafiti, TADIP ni kifupi cha maneno Tanzania Development Ini7a7ves Program. Ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiliwa mwaka 2006.
-Tangu kuanzishwa kwake, TADIP imekuwa ikileta chachu katika maendeleo ya Tanzania kupitia programu yake ya “Maendeleo Dialogue”.
-
Anasema kupitia tafiti na midahalo, TADIP imekuwa ikiwaunganisha wananchi, wanataaluma, asasi za kiraia na watunga sera katika kushawishi michakato mbalimbali ya maendeleo.
-Tangu mwaka 2010, TADIP imekuwa ikijishughulisha na tafiti za kura ya maoni ya wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.
Tafiti za kura ya maoni pamoja na mambo mengine hulenga kujua maoni ya wapiga kura juu ya utayari wao wa kupiga kura, kukubalika kwa wanasiasa katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani, na mitzamo ya wananchi juu ya taasisi na mifumo ya usimamizi wa uchaguzi.
-Katika hatua ya Kura ya Maoni anasema huu ni utafiti wa pili wa kura ya maoni kufanywa na TADIP kuelekea 25 Oktoba, wa kwanza ulifanyika mwezi Mei na Juni 2015. Utafiti huu umefanyika ndani ya wiki tatu za mwanzo za mwezi Septemba.
-Utafiti huu ulilenga wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika mikoa 12 ya Tanzania. Lengo la utafiti lilikuwa mikoa ambayo ina idadi kubwa ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura ka7ka daSari la kudumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa sababu zilizokuwa nje ya Taasisi, taarifa za mikoa 2 hazikuweza kupatikana kwa wakati (Tabora na Kagera)
-Watu 2500 walilengwa kupewa madodoso huku watu 2040 pekee ndo waliweza kushiriki kwa maana ya kurejesha dodoso. utaratibu wa kuchagua washiriki ulifanyika kwa njia ya nasibu (simple randomisation) huku kwa kila mkoa, walengwa wakigawanyika katika makundi matatu ya maeneo, mijini, miji midogo na maeneo ya pembezoni. Methodolojia...
-Aidha, wakusanya taarifa walichagua washiriki kwa kuzingatia uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii kama vile elimu, jinsia, umri, kiwango cha elimu ya washiriki na kadhalika.
-Wahojiwa walipewa madodoso ya wazi (Open ended questionnaire) kwa ajili ya kujaza majibu ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wale waliokuwa hawawezi kusoma na kuandika walisaidiwa kujaza taarifa na wakusanya taarifa.
-Jendwali na 1 hapo linaonyesha mgawanyo wa sampuli katika mikoa husika. Moja ya kigezo kilichotumika kuhoji ilikuwa ni mhusika kuwa amejiandikisha kupiga kura kwenye dasari maalum kwa mfumo wa kielekroniki yaani BVR.
George anatoa matokeo ya utafiti, na kusema matokeo haya yamempa Edward Lowassa kuwa mtu wa kwanza ambaye angechaguliwa kuwa Rais na pia anaelezea jinsi wafuasi wa vyama vya siasa wanavyopenda vyama hivyo ambapo CCM kimeonekana kuwa na wafuasi kwa asilimia 35, Chadema 32, CUF 2, NCCR Mageuzi 1, ACT 3, Vingine 2 na ambao hawana chama walikuwa ni asilimia 25
Pia utafiti uliangalia namna ya jinsi wagombea urais wanavyokubalika.
-Wananchi wangependa serikali ijayo iboreshe hali ya huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, na maji.
Kujenga uchumi imara utakaoboresha hali ya sekta za kilimo na viwanda ili kuleta 7ja ka7ka utoaji wa ajira.
Kusimamia rasilimali za umma na mapambano dhidi ya rushwa .
-Asilimia 97% ya wanachi wana utayari wa kushiriki zoezi la upigaji kura CCM kinaongoza kwa wanachama ama wafuasi kwa asilimia 35% ikifuatiwa na CHADEMA (32%) huku wananchi wasiokuwa na vyama wala ufuasi wakiwa 25%.
-Vyama vingine ni pamoja na ACT 3%, CUF 2%, NCCR-Mageuzi 1% qEdward Lowassa anaungwa mkono zaidi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha huku Dr John Magufuli akiungwa mkono zaidi na wananchi wa mikoa ya Dodoma na Morogoro John Magufuli anakubalika zaidi miongoni mwa wapiga kura wenye umri wa zaidi ya miaka 48 huku Edward Lowassa anakubalika zaidi miongoni mwa wapiga kura wenye umri wa chini ya miaka 47.
-Edward Lowassa angepigiwa kura na wanaume kwa uwingi kuliko wanawake huku Dr. Magufuli na Anna Mghwira wakiwa na uwezekano wa kupigiwa kura zaidi na wanawake ikilinganishwa na wanaume katika nafasi ya Ubunge, 53% ya wahojiwa walisema kuwa wangemchagua mgombea kutoka miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA (CHADEMA, NLD, CUF, NCCR), huku asilimia 40% wakisema wangechagua mgombea kutoka CCM qAsilimia 55 ya wananchi wangechagua mgombea anayetoka ka7ka vyama vya UKAWA ikifua7wa na CCM (37%).
-Vyama vingine ni pamoja ACT (3%), TLP (2%), UDP (0.6%) na asilimia (2.3) hawajafanya maamuzi qEdward Lowassa angeweza kupigiwa kura kwa asilimia 54.5 akifuatiwa na Dr. John Mafuguli 40% ambaye angefuatiwa Anna Mghwira 2.
George, anasema madodoso yao yalifanyika kwa lugha ya Kiswahili na kwamba utafiti utafiti huo waliudhamini wenyewe.
-Anasema bajeti ya utafiti huo ilikuwa Sh. Milioni 10 tu
Wamemaliza kuongea.
No comments:
Post a Comment