Sunday, 20 September 2015

MABASI YA MWENDO KASI YATUA DAR, KUANZA "KUSANYA" ABIRIA MWEZI OKTOBA


Mabasi ya mwendo kasi, yakishushwa kutoka melini kwenye bandari ya Dar es Salaam, leo Septemba 20, 2015. Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT), kuanzaia mwezi Oktoba, 2015, Maafisa wanaosimamia mradi huo wamewaambia waandishi wa habari kagtika hafla ya kuyapokea mabasi hayo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick na viongozi wa DART

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa kuanzahuduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao,kushoto ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT), Robert Kisena ambaye pia ni Mwekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo, Sabri Maburuki

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...