ZIKIWAZIMEBAKIA siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (DED), Saada Malunde amewataka wanawake kudhibiti shahada zao za kupigiakura na wasikubali kurubuniwa kuuza shahada hizo.
Alisema kuwa katika hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu wanawake mara nyingi wanatumika kisiasa na wanasiasa kwa rubuniwa kwa vitu vidogo.
DED huyo alisema hayo wakati akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima mjini Mafinga jana.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Land O' Lakes chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Ubunifu katika Masuala ya Kijinsia na kuimarisha Uhakika wa Chakula katika ngazi ya kaya.
“Mujue kuwa mukizitoa shahada zena itakuwa mumeuza utu wenu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo”, alisema Malunde.
Alisema kuwa wanaweza kuja watu wakataka muwape shahada zenu za kupigia kura, nakunasihini hata kuwaonesha musiwaoneshe achilia mbali kuwapa.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo wa halmashauri ya mufindi walisahi wanawake hao kuzingatia mafunzo hayo kwa kuyatumia kuboresha maisha kwa kulima kilimo cha biashara.
Aliongeza kuwa wanawake mara nyingi wanakabiliwa na upatikanaji mdogo wa, ardhi ya kutosha, zana za kilimo na pembejeo, mikopo, huduma za ugani na ushauri wa kitaalamu na Miundombinu bora na teknolojia mpya.
Naye, Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu katika Masuala ya Kijinsia na kuimarisha Uhakika wa Chakula katika ngazi ya kaya, Dkt. Rose Kingamkono wanawake ni mali muhimu katika maendeleo ya kilimo duniani kote.
Alisema kuwa katika nchi nyingi za Afrika hadi asilimia 80 ya kazi za shamba hufanywa na wanawake.
Pia kaya nyingi zinazojihusisha na kilimo katika nchi zinazoendelea zinaongozwa na wanawake.
“Wanawake wangeweza kuongeza uzalishaji kwenye mashamba yao kwa asilimia 20–30 kama wangekuwa na upatikanaji sawa wa zana za kilimo, pembejeo, na huduma za ugani kama wanaume,” alisema.
Jumla ya washiriki 45 kutoka wilaya za iringa, Mufindi na kilolo wamepatiwa mafunzo ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima.
mwisho
No comments:
Post a Comment