Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi (DED) Saada Malunde akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Land O' Lakes chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID) (Picha na Friday Simbaya)
MALENGO YA SEMINA
Washiriki kufahamu hali ya upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wakulima hasa wanawake.
Kuchambua changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima wanawake.
Mapendekezo ya nini kifanyike ili kuboresha upatikanaji wa huduma za ugani kwa wakulima.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi (DED) Saada Malunde akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga.
Washiriki wakiwa katika vikundi mbalimbali vya majadiliano wakati wa semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa hudumaza ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga.
Mkurugenzi wa Miradi wa Ubunifu katika Masuala ya Kijinsia na kuimarisha Uhakika wa Chakula katika ngazi ya kaya, Dkt. Rose Rita Kingamkono (mwenye braizi jekundu) akifuatilia hotuba kutokakwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mufindi (DED) Saada Malunde akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga.
Wanawake na kilimo nchini Tanzania
Wanawake ni mali muhimu katika maendeleo ya kilimo duniani kote.
Kwa wasitani nguvu kazi yao ni takribani asilimia 43 ya nguvukazi inayohitajika katika kilimo.
katika nchi nyingi za Afrika hadi 80% ya kazi za shamba hufanywa na wanawake.
Pia kaya nyingi zinazojihusisha na kilimo katika nchi zinazoendelea zinaongozwa na wanawake.
Wanawake wangeweza kuongeza uzalishaji kwenye mashamba yao kwa asilimia 20–30 kama wangekuwa na upatikanaji sawa wa zana za kilimo, pembejeo, na huduma za ugani kama wanaume.
Hii ingeweza kuongeza uzalishaji katika kilimo katika nci zinazoendelea kwa asilimia 2.5–4 na
Hivyo kupunguza idadi ya watu wenye lishe duni duniani kote kwa asilimia 12–17%.
Wanawake wanakabiliwa na upatikanaji mdogo wa;
Ardhi ya kutosha, Zana za kilimo na pembejeo, Mikopo, Huduma za ugani na ushauri wa kitaalamu na Miundombinu bora na teknolojia mpya.
No comments:
Post a Comment