Friday, 9 October 2015

COSATO CHUMI AKERWA PROGANDA CHAFU ZINAZOFANYWA NA MPINZANI WAKE!

Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi (CCM) (katikati) akielezea masikitiko yake kuhusu kutoridhishwa na kampeni na propaganda chafu zinazofanywa na mgombea mwenzangu wa Chadema kwa waandsihi wa habari jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni -Jimbo la Mafinga mjini Albert Chalamira na Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Mufindi, Nuru Ngeleja (kulia)


Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa mgombea na waandishi wa habari katika ofisi za chama mjini Mafinga jana

Meneja wa Kampeni -Jimbo la Mafinga mjini Albert Chalamira (katikati) akielezea hali kampeni katika jimbo hilo kwa wanahabari ambapo alisema kuwa CCM inauhakika wa kushinda uchaguzi kwa asilimia 80.

Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi (CCM) akionesha waraka wa kampeni chafu zinazodaiwa kumuzoofisha iliyopewa jina MKAKATI WA USHINDI JIMBO LA MAFINGA MIJINI kwa wanahabari. (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)

Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) amesema ni jambo la aibu, kusikitisha na hata kusononesha kuona kuwa katika wakati huu ambao taifa linaendea kukua na kukomaa katika siasa za vyama vingi na demokrasia ya uwazi na uwajibikaji kuna wanasiasa ndani ya jimbo wanashindwa kufanya siasa za kistaarabu.

Alisema kuwa wapo wanasiasa wanaofanya siasa za maji taka badala ya kuelezea sera, mipango na vipaumbele vya namna gani watakavyolinyanyua Jimbo la Mafinga mjini na badala yake wanaendeleza mbinu chafu za kupakana matope.

Mgombea huyu alisema kuwa hivi karibuni, timu ya kampeni imegundua na kubaini kuwa mgombea mwenzake William Mungai (Chadema) ameadaa waraka wa kurasa nne uliojaa tuhuma na uzushi dhidi ya wagombea wa CCM, kuanzia mbunge, madiwani na mgombea urais.

Kwa mfano, wamekubaliana kupitia waraka huo kuwaaminisha vijana wa bodaboda na bajaji kuwa akichaguliwa atafuta bodaboda, bajaji, atafuta mnada na atawatimua akina mama wauza matunda na mbogamboga.

Pia atawatimua vijana wauza mahindi kandokakdo ya barabara kuu. 

Hata hivyo, alisema kuwa huo ni uzushi mkubwa sasa na kumalizia kwa kutumia msemo wa kiswahili 'kuwa mfa maji hakosi kutapatapa' Usikose kusoma Nipashe kesho!





No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...