Thursday, 1 October 2015

Mke wa Lowassa awapa mbinu za kupiga kura Babati

ticle class="main column">


Thursday, October 1, 2015
Mke wa mgombea urais wa Chadema, Regina Lowassa akizungumza na wanawake katika moja ya mikutano yao. Picha na Maktaba 


Amewataka kutobabaika siku ya uchaguzi kwa kuwa kipindi cha mabadiliko kimefika

By Joseph Lyimo, Mwananchi


Babati. Mke wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina amewaomba Watanzania kuwa makini siku ya kupiga kura, kutunza kadi zao.


Pia, Regina amewaomba wapigakura wasichore wala kuandika chochote kwa mgombea mwingine siku ya kupiga kura ili kuepuka kuharibu kura zao na kumpunguzia idadi ya kura mumewe.


Alitoa ombi hilo juzi, wakati akizungumza na wakazi wa mjini Babati, baada ya kumaliza kuzungumza katika mkutano wa ndani na wanawake.


Alisema ili wasiharibu kura zao baada ya kuwasili asubuhi kwenye kituo cha kupiga kura, wanatakiwa kuweka alama ya vema kwenye eneo la mgombea udiwani, ubunge na urais wa Chadema.


Alisemawananchi wamehamasika na mabadiliko ndiyo maana wana uhakika wa kwenda Ikulu kwa kuwa wanaungwa mkono na makundi ya watu nchini.


Akizungumza katika mkutano huo, mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Babati mjini, Pauline Gekul aliwaomba wapigakura wampigie kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu kwa kuwa aliwatetea alipokuwa mbunge wa viti maalumu. 


























Habari 











2
hours ago
NEC: Kalamu yoyote inaruhusiwa kupigia kura













Ili kuondoa shaka miongoni mwa wananchi kutokana na tetesi zinazosambazwa juu ya ubora wa kalamu

2
hours ago
Polisi yathibitisha mgombea ubunge wa ACT kutekwa













Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutekwa kwa mgombea ubunge Jimbo la Bariadi, kupitia










Kitaifa 
Mashahidi 50 kutoa ushahidi mauaji ya bilionea Msuya 5
hours ago



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...