Rais Mteule Dkt. Magufuli
Ndugu zangu watanzania, uchaguzi umeisha, rais, wabunge na madiwani wameshapatikana katika uchaguzi mkuu 2015. Tusiendeleze siasa wala ushabiki usio na tija maana viongozi waliochaguliwa ni wetu sote na ni viongozi wa taifa la Tanzania.
Rais John Phombe Magufuli alikuwa anaeleza mara zote kwenye mikutano ya kampeni kwamba akichaguliwa atakuwa rais wa watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, dini au rangi kwahiyo hatutegemei kwamba kuna mtu mwenye hatimiliki na urais wa Magufuli.
Kama kuna makovu yaliyotokana na pilikapilika za kampeni, huu ni wakati wa kuyaponya na kuanza maisha mapya ya kuijenga Tanzania. Malumbano ya kisiasa, vijembe na kejeli sasa basi, tufungue ukurasa mpya wa kuimarisha umoja na mshikamano kwa maendeleo ya taifa maana hakuna mtu atakaetafuta uraia wa nchi nyingine, kisa kushindwa kwa mgombea au chama alichokuwa anakiunga mkono.
Hongera Magufuli, Tanzania kwanza, Tanzania ni ya watanzania na Tanzania ni yetu sote.
No comments:
Post a Comment