Baadhi ya washiriki wa warsha iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo ya Kale wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mr Adelhelm Meru kufungua warsha hiyo iliyofanyika Coral Beach jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya viongozi wa Hifadhi wakifuatilia warsha hiyo iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo ya Kale
Mwakilishi wa UNESCO Nchini Ms Zulmira Rodriguez (katikati) akichangia moja ya mada iliyowasilishwa na baadhi ya wakuu wa hifadhi waliohudhuria warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dr Adelhelm Meru akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya Mambo ya Kale kwaajili ya kujadili uboreshwaji wa utawala na matumizi endelevu ya hifadhi za urithi na mazingira za Tanzania, ambazo ni Magofu ya Kilwa; Michoro ya Asili Kondoa; Mji Mkongwe Zanzibar; Hifadhi ya Wanyama Selous; Hifadhi za Taifa za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara na Mlima Kilimanjaro; na Hifadhi ya Mazingira ya Usambara Mashariki’.
Mkuu wa Hifadhi ya Kondoa Rock Art, Zuberi Mabie akichangia mada katika warsha hiyo iliyofanyika jana katika kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili hifadhi hizo.
Warsha ikiendelea juu ya utunzaji na uendelezaji wa maliasili na vivutio vya Utalii iliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach jijini Dar Es Salaam
Na Josephat Lukaza
UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii hapa nchini huku wakuu hao wakishirikishana mafanikio na changamoto zinazowakabili katika hifadhi zao
Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali hapa nchini iliweza kuhusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wakuu wa hifadhi hizo katika hifadhi huku matatizo makubwa yakiwa ni Ukosefu wa Pesa kwaajili ya Kujiendesha na Kwa baadhi ya hifadhi kukosa nyumba za Wafanyakazi na upungufu wa wafanyakazi kwa baadhi ya hifadhi hizo.
Mbali na Changamoto hizo pia wakuu wa hifadhi walielezea mafanikio yao katika hifadhi hizo katika vipengele tofauti tofauti kama Vitendea kazi, Ujumuikaji wa jamii katika hifadhi hizo, Utalii, Rasilimali watu, Uhifadhi Utawala na mengineyo.
Moja ya mafanikio katika nyanja tofauti Mkuu wa Hifadhi ya Usambara Mashiriki (East Usambara Reserve Management) Bi Mwanaidi Kijazi alisema kuwa hifadhi yake imetokea kuwa kituo cha Mafunzo kwa wengine na kupelekea kuanzishwa kwa Amani Nature Reserve na hifadhi hiyo kufanikiwa katika kutoa taarifa kwa wakati kwa njia ya Vipeperushi kuhusiana na Mradi huo wa Amani Nature ambao upo kusini mwa Hifadhi hiyo ya Usambara Mashariki.
Vilevile alisema katika hifadhi yake kuna wafanyakazi ambao wanaweza kuhudhuria shughuli za Hifadhi hiyo na kusema na hiyo ni moja ya Mafanikio katika Hifadhi hiyo ya Usambara Mashariki.
Kwa Upande wao UNESCO walisema wataendelea kushirikiana na idara ya Mambo ya Kale katika kutoa ushirikiano na misaada ya kitaalam katika kuhakikisha Hifadhi hizi zinaweza kujiendeleza na kujiboresha na kuvutia watalii zaidi.
No comments:
Post a Comment