Thursday, 19 November 2015

'Matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa bado vipo chini'

IRINGA: JUMLA ya kaya 201,120 ambayo ni sawa na asilimia 89 mkoani Iringa zina vyoo na kati ya Kaya hizo asilimia 17 tu ndiyo zenye vyoo bora. 

Kauli hiyo imetolewa jana na katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo ya kuhamamisisha wanahabari juu ya usafi wa mazingira.

Ayubu alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwa kuwajengea uwezo wanahabari kujua mambo muhimu yanayohusiana usafi wa mazingira na matumizi ya choo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.

Alisema kuwa hali ya unawaji mikono kwa sabuni ni sawa na asilimia tisa huku hali ya matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa bado vipo chini.

Naye ofisa afya wa mkoa wa Iringa Khadija Haroun alisema mafunzo hayo yanaenda sambamba na wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.

Haroun alisema kuwa watu takriban milioni 1.8 wanakufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya kuhara.

Alisema kuwa watoto chini ya miaka mitano 760,000 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara kila mwaka.

Pia alisema kuwa tanzania watu 30,000 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara.

“Asilimia 60 hadi 80 ya wagonjwa wote wa nje wana magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji na mazingira machafu.”alisema Haroun

Aliwataka wananchi kuonya matunda kabla ya kula ,kunawa mikono kwa maji safi na sabuni mara baada ya kutoka chooni ili kuepukana na magonjwa hayo ya kuhara.

Naye Ofisa habari wa mkoa wa Iringa Dennis Gondwe aliwataka wanahabari mkoani hapa kutoa elimu kwa jamii kuhusu mafunzo waliyoyapata katika mafunzo hayo ambapo alisema kwa kupitia waandishi wa habari jamii itapata elimu itakayowasaidia kuweza kuepukana na ugonjwa wa kuhara pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.

MWISHO

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...