Friday, 27 November 2015

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA KUJULIKANA DESEMBA 2



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa mjini kimekanusha vikali kuwapo kwa mvutano katika mchakato wa kumpata meya atakayoongoza baraza la halmashauri ya manispaa ya Iringa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Wakizungumza na wanahabari jana mjini hapa Mwenyekiti wa wilaya ya Iringa mjini Frank Nyalusi na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema na mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa pamoja na madiwani wateule wa chama hicho, Nyalusi alisema kuwa habari iliyoandikwa na moja ya gazeti la kila siku la hapa nchini ni uzushi na wa kupuuzwa.

Nyalusi amesema kuwa hawawezi kupuuza kila wanachoambiwa maana hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu hovyo waulizeni walipomtoa huyo meya wanayetuletea na kwanini ni huyo na siyo wale waliokuwa wakitajwa tajwa na ccm wasahau kabisa kumpata meya katika baraza la madiwani.

Amesema kuwa uzushi huo umeendikwa kwa lengo la kuuza magazeti hivyo jamii inapaswa kusubiri jina ambalo litapitishwa na kamati kuu kuweza kuongoza halmashauri kwa kuwa chama kimetekeleza majukumu yake ya kuweza kumpata mgombea umeya ambaye atapatikana kutokana na miongozo na taratibu za chama.

Pia amesema kuwa majina ya wagombea wa Umeya na Naibu Meya yamepelekwa katika kamati kuu ambayo itachuja kati ya majina matatu katika kila nafasi na kupata jina moja ambalo litasimamishwa kugombea nafasi hizo.

Naye mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amesema kazi ya chama Jimbo ilikuwa kupendekeza jina la mgombea na kuliwasilisha kwenye kamati kuu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuteua mgombea.

Hata hivyo msigwa aliwaomba wakazi wa mji wa Iringa na viunga vyake kujitokeza kwa wingi Desemba 2 mwaka huu kwani siku hiyo ndiyo watakayoapishwa madiwani hao na kuongeza historia itaandikwa kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Iringa kwa baraza hilo jipya kuendeshwa katika viwanja vya wazi na kutaja kuwa litafanyika katika bustani ya manispaa itatumika katika vikao au ukumbi mkubwa zaidi kuweza kuwapa nafasi wananchi kusikiliza baraza hilo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...