Waziri wa madini nchini Profesa Sospeter Muhongo aliye wasili mkoani Iringa Siku ya Jana na kutembelea vijiji kadhaa mkoani humo.
Muhongo amewasili Iringa akitokea Pangani mkoani tanga lengo ni kuangalia hali ya vyanzo vya maji vinavyozalisha Umeme
Akipokewa na mwenyeji wake ambaye ni mkuu Wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela na kutembezwa baadhi ya vijiji vilivyopo Pawaga na Isiman panapo unganisha bwawa la mtera
Kwa mujibu Wa Kasesela amesema hali ya bwawa la mtera ni mbaya kwani maji yamekauka na kusababisha ukaukaji Wa maji
Hali hiyo imemfanya Pr. Muongo kuagiza kufanyika kwa kikao cha wadau Wa maji, misitu, Tanapa, wavuvi nk mapema kutafuta suluhisho la janga hilo
Kasesela amesema atafanya kikao hicho mapema Juma tatu ya wiki ijayo ofisini kwake mawelewele na baadae kuelekea mtera.
No comments:
Post a Comment