IRINGA: Diwani wa Kata ya Gangilonga Jimbo la Iringa Mjini, Dady Igogo (Chadema) pichani ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima katika kuhakikisha kuwa fedha zinaelekezwa katika miradi ya kimaendeleo.
Diwani huyo alisema kuwa posho za vikao ni ugonjwa wa ufisadi unalolitafuna taifa hili hususan kwa watendaji wa mashirika ya umma, watendaji wa serikali kuu, wabunge na madiwani.
Akizungumza na SIMBAYABLOG mjini Iringa leo diwani huyo alisema kuwa anayo dhamira ya dhati yakuazimia kutopokea posho za vikao kwa kipindi cha miaka mitano ya utumishi wake, na badala yake posho hizo zielekekezwe kwenye eneo la kusaidia vituo vya watoto yatima.
Alisema kuwa katika kuunga mkono Rais Magufuli wa awamu ya tano ameamua kutopekea posho za vikao kwa kipindi cha miaka mitano ya utumishi wake, na badala yake pesa hiyo zisaidie watoto yatima kwenye Kata ya Gangilonga.
Alisema kuwa suala hilo tayari amewasilisha kwenye kamati ya maendeleo ya kata ya Gangilonga ambapo lilipokelewa, na hatimaye iliundwa kamati itakayokuwa ikiratibu posho hizo ambao ni; mwenyekiti wa mtaa wa kichangani, mwenyekiti wa mtaa kinondoni na mtendaji mmoja wa mtaa.
“Naamini kuwa udiwani siyo kazi ya ajira, bali ni kazi ya utumishi kwa wananchi waliokuamini na pia kuwa miongoni mwa majukumu ya udiwani ni pamoja na kukaa vikao,” alisisiza.
Alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya iringa asilimia 34 ya mapato yake inategemea serikali kuu pamoja na wahisani kwa vilie uwezo wake ni shilingi bilioni nne (4bn/-)tu makusanyo ya ndani (own source), sawa ni asilimia 16.
Alisema kuwa ili halmashauri iweze kujitegemea kimapato ni lazima itafute vyanzo vya mapato mbadala ili ni pamoja na kupunguza matumizi ya siyo ya lazima.
Alisema kuwa wastani wa posho za madiwani na watendaji kwa mwaka mmoja katika manispaa ya iringa ina uwezo wa kusomesha wanafunzi zaidi ya 4000 wa shule za sekondari.
“Nikiwa sehemu ya historia hii muhimu ya kuwa diwani wa kwanza Tanzania kukataa posho, naomba ni kuchukuwa fursa hii kuwaomba madiwani wenzangu pamoja mbunge wa iringa mjini, na mbunge viti maamlumu wa iringa kuwa sehemu ya kupinga uendelezaji wa posho zisizokuwa za msingi, ” alisema diwani huyo.
Alisema pia ni msimamo wa chama chake katika ilani yake ya uchaguzi kwa mwaka 2010 na ilani ya mwkan2015 ya kutaka posho ya kitako au vikao iweze kuftwa.
Kata ya Gangilonga ina idadi ya kaya 2,490, idadi ya watu 9,599 na ina vituo viwili vya watoto yatima ambavyo ni Upendo na Matumaini. (NA FRIDAY SIMBAYA)
No comments:
Post a Comment