RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amemuapisha Waziri wa Fedha na Mipango pamoja na mawaziri wengine wawili na naibu waziri mmoja Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Desemba 28, 2015 na hivyo kukamilisha baraza lake la mawaziri.
Walioapishwa leo ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambaye awali alikuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA).
Wengine walioapishwa ni Profesa Jumanne Maghembe, ambaye anakuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Joyce Ndalichako anayekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Injinia Gerson Hosea Lwenge anayekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, wakati Injinia Hamad Masauni kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Rais amekamilisha baraza lake la mawaziri lenye jumla ya mawaziri na naibu mawaziri 34 ikiwa ni nusu ya idadi ya baraza la mawaziri al serikali ya awamu ya nne ya Dkt. Jakaya Kikwete. (Picha juu Dkt. Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Mpango. (Picha zote na MAELEZO)
Dkt. Magufuli akimuapisha Profesa Jumanne Maghembe
Dkt. Magufuli akimuapisha Dkt. Joyce Ndalichako
Dkt. Magufuli akimuapisha Injinia Gerson Lwenge
Dkt. Magufuli akimuapisha Injinia Hamad Masauni
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
No comments:
Post a Comment