Wednesday, 9 December 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WANANCHI WA KILOLO WALIA KERO YA MAJI


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo, Rukia Muwango akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi likiwemo la maji.




 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (kushoto) akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali wakielekea eneo la kufanyia usafi.










Wananchi wa Mkoa wa Iringa wameungana na Watanzania wengine kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya usafi kwenye maeneo wanayoishi na wanakofanyia kazi huku wakipongeza hatua hiyo ya Rais kuwa anatekeleza kwa vitendo azma ya kupambana na maadui watatu wa maendeleo ikiwemo ujinga, umaskini na maradhi.

SIMBAYABLOG tukiwa njiani kuelekea katika Kijiji cha Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo umbali wa zaidi ya kilometa 100 kutoka Iringa mjini tunakutana na wananchi waliojitokeza kufanya usafi maeneo wanayoishi kando kando ya barabara Kuu ya Iringa –Dar es Salaam.

Wananchi hawa wamejihimu kufanya usafu tangu saa 12 asubuhi kuanzia majumbani kwao hadi mitaani.

Barabara Kuu ya Iringa –Dar es Salaam huwa na takataka nyingi za makopo ambayo hutupwa na abiria wanaosafiri lakini leo eneo lote linaonekana ni safi.

Pamoja na wananchi kupongeza hatua hii ya usafi wana kilio cha maji ambayo ni chachu ya usafi..

Akizungumza na wananchi wa Ruaha Mbuyuni, Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiongozana na viongozi mbalimbali serikali walishiriki na wananchi kufanya usafi na kuwataka kulifanya zoezi hilo liwe endelevu huku akiwaagiza watendaji kuhakikisha wananchi wanajenga vyoo bora kuepuka magonjwa ya mlipuko.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...