Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wa watendaji wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida mara tu alipowasili kijiji cha Puma kukagua mradi wa ufugaji kuku wa kusaidia watu wanaoishi na VVU unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia TACAIDS. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Na Modewjiblog team, Singida
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Bw.Alvaro Rodriguez ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira yanayofanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu.
Mratibu huyo alitoa wito huo wakati alipofanya ziara ya siku mbili mkoani Singida kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Baada ya kuona mafanikio katika miradi hiyo Bw. Rodriguez, alisifu pia jamii ya Singida kwa kujitoa kuhakikisha kwamba wanafanikisha miradi hiyo kwa kuifanya kuwa miradi yao.
Katika ziara hiyo ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah Hassan walikuwepo, Mratibu alitembelea kituo cha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi; Kituo cha kutibu kipindupindu na Ushirika wa wajasiriamali vijana.
Miradi hiyo inafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS).
UNAIDS ni mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mashirika ya TACAIDS na ZAC.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Puma kukagua mradi wa kikundi cha ufugaji kuku kwa watu wanaoishi na VVU.
Mashirika ya TACAIDS na ZAC yanatambulika kitaifa na kimataifa kutokana na shughuli zake za kuhudumia umma wa Tanzania.
Miradi hiyo imewezesha vijana wengi kuwa wajasiriamali, kudhibiti Kipindupindu na kuongeza uelewa wa UKIMWI.
Alisema kwamba maendeleo endelevu yanahusisha serikali na jamii kuangalia changamoto zinazokabili jamii na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuoanisha na malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Miradi hiyo iliyopo Singida inatekelezwa chini ya mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanywa shughuli mbalimbali za kusaidia wananchi wa Tanzania waume, wake na watoto kupitia mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP) wa mwaka 2011-2016.
Naye Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Kone akisisitiza umuhimu wa wananchi kujimilikisha miradi hiyo, amewaambia Umoja wa Mataifa kwamba kwamba wananchi wa mkoa huo wataendelea kujimilikisha miradi hiyo na kuifanya ya kwao ili kuharakisha maendeleo endelevu.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Chigulu Charles (wa kwanza kulia) akitoa taarifa yake ya mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI wilayani humo. Wa tatu kushoto,ni Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone.
Alisema maelfu ya wananchi wa Singida wamenufaika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake yaliyopo hapa nchini .
Aidha alitaka Mashirika hayo kuendelea kusaidia miradi mbalimbali na hasa wakati Mpango wa pili wa Msaada wa maendeleo (UNDAP II) unapokaribia kuanza mwakani, sanjari na mpango wa maendeleo wa taifa Julai 2016.
Alisema Singida imesonga mbele katika maendeleo katika siku za karibuni lakini bado inahitaji msaada wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuhifadhi mafanikio na kuyaboresha.
Mhudumu wa watu wanaoishi na VVU kata ya Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, Kelvin Mwiru, akitoa taarifa yake juu ya majukumu ya kuhudumia watu 150 wanaoishi na VVU katika vijiji vya kata ya Puma na vijijini jirani.Mhudumu huyo ameiomba halmashauri ya wilaya ya Ikungi na wadau wengine kumtambua na kumpa ushirikiano katika kazi hiyo ngumu ya kujitolea kuwahudumia watu wanaoishi na VVU ambao wanaongezeka kila kukicha.
Mratibu mkzi wa mashirka ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (anayengalia kamera) akitoa nasaha zake mbele ya kikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU na wananchi kwa ujumla wa kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi.Mwenye suti ya bluu, ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone wakiangalia baadhi ya kuku wa mayai walipotembelea kikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU na wananchi kwa ujumla wa kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kulia) pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (katikati) wakitazama mayai yanayototolewa na kuku hao.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone, Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Chigulu Charles (kulia), Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan na Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akiondoka katika kijiji cha Puma kuelekea kijiji cha Mandewa kilichopo Singida mjini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mganga mfawidhi wa manispaa ya Singida, Dk. John Mwombeki baada ya kuwasili kwenye kambi ya muda ya wagonjwa wa Kipindupindu iliyopo katika kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida akiwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiingia kwenye kambi ya muda ya wagonjwa wa kipindupindu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni katika kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwaeleza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) na Afisa kutoka Shirika la Afya (WHO) kanda ya Dodoma, Dk. Cyrialis Mutabuzi (kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akizungumza na mgonjwa wa kipindupindu kutoka kijiji cha Mtavila wilaya ya Ikungi, Jumanne Shaban. Dkt. Kone amemuagiza akirudi kijijini akawe Balozi mzuri wa mapambano dhidi ya kipindupindu.WHO inasaidia uendeshaji wa vituo hivi pamoja na tiba.
No comments:
Post a Comment