Wednesday, 13 January 2016

BAADHI YA VIONGOZI WA MANISPAA YA IRINGA WAPANDA MITI KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA NDULI

 diwani wa kata ya nduli bashiri  mtove na mbunge wa jimbo la irirnga mjini mch. petter msigwa wakibalishana mawazo baada ya zoezi la upandaji wa miti katika shule ya sekondari ya nduli.
mkuu wa wilaya ya iringa richard kasesela akibanda mti katika shule ya sekondari  ya kihesha wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira

 diwani wa kata ya mivingeni akibanda mti katika shule ya sekondari  ya kihesha wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira

 mbunge wa jimbo la irirnga mjini mch. petter msigwa akibanda mti katika shule ya sekondari  ya kihesha wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira
 diwani wa kata ya kihesa edger mgimwa akibanda mti katika shule ya sekondari  ya kihesha wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira

  mbunge wa jimbo la irirnga mjini mch. petter msigwa akibanda mti katika shule ya sekondari  ya kihesha wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira
 diwani wa kata ya isakalilo ambaye ndio meya wa halmashauri ya iringa alex kibe akinawa mikono baada ya kupanda mti katika shule ya sekondari ya nduli
 diwani wa kata ya kihesa edger mgimwa na diwani wa kata ya nduli bashiri  mtove wakinawa mikono baada ya kupanda miti katika shule ya sekondari ya nduli

na mwandishi wetu,iringa

viongozi wa manispaa ya iringa wamepanda miti zaidi ya elfu mbili miatatu(2300) katika shule ya sekondari ya nduli iliyopo kata ya nduli mkoani iringa.

mkuu wa wilaya ya iringa richard kasesela aliitumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wote wa wilaya ya iringa kutenga maeneo maalum ya kupanda miti kwa ajili ya watu wasiojiweza.  
Miti hiyo itachangia baadaye katika upatikanaji wa fedha za kuwasomesha watoto wa familia hizo. 

Vilevile mkuu wa wilaya ya iringa richard kasesela amezitaka halimashauri zote kustawisha miche ya kutosha na kuwapatia wananchi waipande kwa wingi kwa nia ya kuifanya miti kuwa zao maalum la uwekezaji katika wilaya hiyo. 
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya iringa richard kasesela amewataka wanafunzi kuipalilia miti inapokuwa midogo, kuitunza kitaalam na kuilinda dhidi ya moto kichaa.
Naye mbunge wa jimbo la iringa mjini mch. Petter msigwa amewaomba walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi juu ya umuhimu wa miti na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Bashiri mtove ni diwani wa kata ya nduli amewashukuru viongozi waliohudhuria tukio hilo la upandaji miti katia shule ya sekondari ya nduli na kuwaomba wanafunzi na wananchi waliojitokeza katika eneo hilo kuitunza na kuthamini miti walioipanda kwani ni hadhina ya miaka mingi ya baadae.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya nduli amewapongeza viongozi wote waliohudhuria kupanda miti katka eneo hlo na kuwaahidi kuitunza miti hiyo na kuongeza miti mingine ili kuifanya shule hiyo kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa ya kijani muda wote.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...