Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo lenye namba za usajili T 782 ACR aina ya Scania linalofanya safari za Dar es salaam - Njombe limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar, baada ya kugongana na lori yenye namba za usajilli T 718 CRV aina ya IVECO.
Lori hilo lilikuwa linatokea Songea kwenda Dar likiwa limebeba makaa ya mawe.
Inasadikika limeua baadhi ya abiria na majeruhi ni wengi. Ajali imetokea maeneo ya Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa (Mufindi).
====
Hadi sasa, waliothibitika kupoteza maisha ni wanne na wengine 32 kujeruhiwa kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali ya Mafinga Innocent Mhagama.
Waliofariki dunia ni Rashid Kibalala,47 ambaye alikuwa ni kondakta wa basi, Salim Chamgwila, 28 ambaye alikuwa mkaguzi wa tiketi (inspekta) na maiti mbili bado hazijatambulika.

No comments:
Post a Comment