Monday, 8 February 2016

ASKARI WALIOFARIKI MSAFARA WA RAIS MAGUFULI WAAGWA SINGIDA



Askari watatu wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, waliofariki dunia wakiwa kwenye msafara wa rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya gari lao walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na dereva kushindwa kulimudu wakitokea Singida kuelekea Dodoma wameagwa jana. Zifuatazo ni picha za tukio hilo la kuaga miili ya askari hao.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, akitoa salamu za pole kutoka kwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini, Ernest Mangu na polisi mkoa wa Singida kwa familia za askari polisi watatu waliofariki dunia wakati wakiwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli jana kutoka Singida Dodoma.


Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Manyara, ACP Camilius Wambura, akitoa salamu za pole kwa familia na jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na askari polisi watatu waliokuwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli wakitokea Singida kuelekea Dodoma juzi.


Mkuu wa mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone, akitoa salamu za pole kwa familia na jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na askari 3 kwenye ajali iliyotokea Isuna kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli uliokuwa ukitokea Singida kuelekea Dodoma juzi.


Askari polisi mkoa wa Singida,wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Insp.Miraji mwigelo Kindamba,Insp.Kindamba ni moja kati ya askari 3 waliofariki juzi kwenye ajali iliyotokewa kwenye msafara wa Dk. Magufuli uliokuwa ukitokea Singida kwenda Dodoma.


Baadhi ya mamia ya waombolezaji wa msiba mkubwa wa askari polisi watatu waliofariki juzi wakiongoza msafara wa rais Dk.Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma.(Picha zote na Nathaniel Limu)

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...