Mchungaji wa Daily Bread Life Ministries Tanzania (DBL), Neema Mpeli Mwaisumbe (kulia) akikabidhi msaada wa madogoro 15, mablanketi 10 and mashuka 10kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza kwa ajili ya waathirika wa mafuriko huko Pawaga. (Picha na Friday Simbaya)
Mchungaji wa Daily Bread Life Ministries Tanzania (DBL), Neema Mpeli Mwaisumbe ambaye aliongozana na mratibu wake Mchungaji Pawde Scout Mwasanje wamekabidhi msaada wa magodoro 15, mablanketi 10 na mashuka 10 wenye thamani ya laki saba na sabini (770,000/-)leo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko wa Pawaga na Mbolimboli, Iringa Vijijini.
Shirika la hilo la kidini la Daily Bread Life ambalo linaongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mchungaji Mpeli Mwashumbe limekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa niaba ya waathirika wa mafuriko wa Pawaga na Mbolimboli, Iringa Vijijini mkoani Iringa.
Shirika hilo pia lina kituo cha kulelea watoto yatima cha Daily Bread Life Children's Home chenye watoto 40 kilichoanzishwa mwaka 2005 kupitia Daily Bread Life Ministries ambacho kipo Mkimbizi Iringa mjini.
Hivi karibuni WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa.
Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo yalibomoa zaidi ya nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko na kuwapa pole wananchi hao (Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela hivi karibuni inaonesha jumla ya kaya 145 zilizoathiriwa na mafuriko hayo kwa makazi yao kuharibiwa zinahitaji msaada ili kurudi katika maisha yao ya kawaida.
No comments:
Post a Comment