Sunday, 28 February 2016

MBEYA CITY FC WAAGA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO




TIMU ya Mbeya City FC Jumamosi hii imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea katika mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora.

Jumamosi Februari 27, kulikwa na michezo nane iliyochezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo, Mwadui FC ilicheza na maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons ilicheza na Mbeya City na kubamizwa bao 2-1 katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jijini hapa. 

Kwa mantiki hiyo Mbeya City FC imetolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa an Tanzania Prisons bao 2-1, na kufanya Tanzania Prison kusonga mbele katika hatua nyingi ya michuano hiyo katika uwanja sokoine uliyojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha.

Kutokana na hali hiyo wachezaji walicheza chini ya viwango kutokana na uwanja huo kuteleza na kufanya wachezaji wa timu zote mbili kushindwa kuonyesha kandanda safi.

Katika mchezo huo, Tanzania Prisons ilianza kupata goli baada ya kuchungulia katika nyavi ya Mbeya City FC kupitia kwa mshambuaji machachali Mohamed Mkopi katika kipindi cha kwanza.

Hadi mapumziko timu ya Tanzania Prisons ilikuwa inaongoza na kipindi cha pili kulipofika timu ya Mbeya City ilisawazisha kupitia winga wake wa kushoto, Joseph Mahundi baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Haruna Moshi.

Timu zote ziliendelea kukamiana kipindi chote cha pili ndipo mshambuaji mahili Benjamin Asukile wa timu ya Tanzania Prisons alipopiga shuti kali kutoka katikati ya uwanja na kufunga goli la pili katika dakika 82.

Kosa alilofanya mlinda mlango wa Mbeya City, Beno Kakulanya ni kuacha mpira kudunda uliyomzidi urefu na kutumbukia nyavuni.

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Selemani Kinugani toka Morogoro akisaidiana na John Kanyenye toka Mbeya na Milambo Tshikungu toka mkoani Tanga. 

Hata hivyo mzunguko huo wa nne utakamilika leo Jumapili ambapo Simba SC watakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...