Saturday, 20 February 2016

SERIKALI YA KIJIJI YAKAMATA MBAO ZILIKATWA KATIKA MSITU WA GANGALAMTUMBA

NA DENIS MLOWE, IRINGA VIJIJINI

SERIKALI ya kijiji cha Mfyome, kata ya Kiwele katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa imefanikiwa kukamata shehena ya mbao 298 zinazosadikiwa kukatwa kutoka kwenye msitu wa Gangalamtumba uliopo kijijini hapo na kusababisha uharibifu mkubwa wa kimazingira.

Wananchi hao kwa kwa kushirikiana na Chama Cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kupitia mradi wake wa ushiriki wa wananchi katika kusimamia maliasili unaofadhiliwa na Watu wa Marekani (USAID)imefanikiwa kukamata shehena ya hizo zenye thamani ya shilingi miloni 8 baada ya kupatiwa mafunzo ya ufuatiliaji uwajibikaji katika jamii kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kukamatwa kwa mbao hizo katika kijiji cha Mfyome, Afisa Mawasiliano wa LEAT, Miriam Mshana alisema elimu ya uwajibikaji katika jamii ni muhimu kwa vile inasaidia kuongeza hamasa miongoni mwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozungukwa na rasilimali kuweza kuzilinda.

Alisema kuwa Leat kwa kushirikiana na USAID waliwapatiwa mafunzo wanakijiji ambapo mradi huo unawafikia katika kuwawezesha kutambua uwajibikaji katika jamii kwa wananchi katika uhifadhi wa mazingira ambapo juhudi kubwa inafanyika katika kuwadhibiti watu ambao wanaharibu mazingira na kuwachukulia hatua kali.

Mshana alisema kuwa katika miaka ya nyuma jukumu la kutunza misitu, wanyamapori na uvuvi lilikuwa linafanywa na Serikali lakini hivi sasa jukumu hilo limepelekwa katika ngazi ya vijiji na wilaya ambapo wananchi wanashiriki moja kwa moja katika utunzaji wa rasilimali husika na kupatiwa mafunzo sahihi ya utunzaji wa mazingira.

Kwa upande Chuki Mduda ambaye ni mjumbe wa kamati ufuatiliaji uwajibikaji katika jamii katika ngazi ya wilaya amesema baada ya kukamatwa kwa mbao hizo uongozi wa kijiji umeamua mbao hizo zitumike kutengenezea madawati ili kumaliza tatizo la uhaba wa madawati kijijini hapo.

Alisema mbao hizo zimetokana na miti ya asili iliyoko katika msitu wa msitu wa Gangalamtumba ulioko katika kijiji cha Mfyome walikutwa nazo waaribifu wa mazingira baada ya wananchi wengi kupatiwa elimu ya mazingira na kuanza kulinda msitu huo.
Alisema kuwa kwa sasa wananachi baada ya kupatiwa elimu wamekuwa wakiwakamata watu wanaoharibu mazingira na kuwapeleka katika uongozi wa Serikali ya mtaa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi.

Mradi wa ushiriki wa wananchi katika kusimamia maliasili unaosimamiwa na LEAT kwa uadhili wa shirika la maendeleo la kimataifa la Marekeni (USAID) unatekelezwa katika vijiji 32 kutoka halmashauri mbili za Iringa vijijini na Mufindi mkoani Iringa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...