Monday, 15 February 2016

WAKULIMA MBOZI WALIA NA MBEGU FEKI

Na Esther Macha,Tunduma

MAWAKALA wa forodha wanaotoa huduma kwa wateja katika mji wa Tunduma Mkoani Mbeya wameonywa kuacha lugha chafu mbazo zinaweza kukimbiza wageni toka nje ya nchi wanaofika katika mpaka huo kupata huduma .

Hayo yamesemwa jana na ofisa elimu kwa mlipa kodi wa mamlaka ya mapato (TRA)Mkoa wa Mbeya , Kissa Kyejo wakati wa semina ya uhamasishaji na sheria na taratibu katika shughuli za mawakala wa forodha na viongozi wa TRA.

Alisema kuwa mawakala wote wa forodha ni muhimu kuwa na lugha nzuri kwa wateja kwani mpaka huo umekuwa ukitoa huduma kwa wageni mbali mbali .

“Sehemu kama hii ambayo ina mchanganyiko wa watu na wanaotoka maeneo mbali mbali hapa nchini muhimu samba lugha nzuri ikatumika kwa wateja kwani vinginevyio tutapoteza wageni wengi wanaotoka nchi za jirani”alisema Ofisa huyo

Kwa upande wake Ofisa Mfawidhi wa forodha wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)Mkoa wa Mbeya ,Cosmas Magori alisema katika utendaji ni vema kila wakala wa forodha kufuata misingi na taratibu za kazi ili kuweza kujiletea nidhamu ya kazi.

Alisema kuwa mambo muhimu yaliyokuwepo katika semina hiyo ni pamoja na huduma bora kwa wateja,uvaaji wa sare na vitambulisho lengo likiwa ni kuboresha huduma hasa wageni wa nje na ndani ya nchi .

Akizungumzia kuhusu rushwa ,Magori alisema hatapenda kuona kitengo cha forodha wanakuwa vinara wa kuombna rushwa kwa wageni na madereva wanaofika kwao kuomba huduma.

“Naombeni mbadilike katika hili sitapenda kusikia wageni wakilalamikia suala la rushwa kuanzia leo hili lianze utekelezaji mapema ,tufuate maadili ya kazi ili kulinda heshima “alisema Meneja Magori.


Na Esther Macha, Mbeya

SHIRIKA la Ugavi wa umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Mbeya limesema kuwa katika mwaka ujao wa fedha litaanza mchakato wa kubadilisha na kuifanyia marekebisho miundombinu ya umeme ya zamani ili kuendana na mahitaji ya sasa.

Akizungumza juzi kwenye mkutano wa Tanesco na wateja wakubwa wa huduma ya umeme jijini hapa Meneja wa Tanesco mkoani Mbeya Mhandisi, Francis Maze alisema kuwa shirika hilo limedhamiria kutoa umeme wa uhakika katika kipindi kisichozidi miaka miwili kuanzia mwezi julai mwaka huu.

Alisema katika mwaka wa fedha 2016/2017 shirika hilo limetoa kipaumbele kubadilisha mifumo ya miundombinu ya zamani kwa sababu ina inashindwa kuhimili kiwango cha umeme kinachotumika sasa kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wa huduma hiyo mkoani Mbeya.

“Mkoa wa Mbeya una mfumo wa zamani wa kusambaza umeme tunatakiwa kufanya marekebisho makubwa, nyaya zilizizopo ni ndogo haziendani na mahitaji ya umeme yanayohitajika kwa sasa, hivyo kuanzia julai baada ya kuanza mwaka wa fedha tutaanza zoezi hilo na inaweza kutuchukua miezi 24 kumaliza lakini tumeandaa mkakati angalau tutumie miezi 12 kumaliza” alisema.

Maze alisema Tanesco itatoa tenda kwa wakandarasi Binafsi kufanya kazi hiyo ili kuweza kumaliza kwa muda uliopangwa na kwamba watangaza tenda kubla ya mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumzia hali ya umeme mkoani hapa alisema kuwa upo wa uhakika kwa sasa baada ya kufunga Transifoma mpya ya megawati 60 kwenye kituo kikubwa cha Mwakibete kilichopo Sae jijini Mbeya.

Alisema kabla ya mwezi Augusti mwaka huu wataboresha miundombinu inayopeleka umeme viwandani, ikiwa ni pamoja na kubadilisha nguzo ili wawe na hali bora ya umeme kwa kuwa wao ndio wateja wakubwa wa Tanesco.

Kwa upande wake Meneja wa umeme wa kiwanda cha Sementi cha Mbeya ambao kwa mujibu wa Tanesco ni walipaji wakubwa wa umeme mkoani Mbeya Daud Rwebangila alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni kupata umeme ambao haujatulia hali inayowawia vigumu kwenye shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.

Alisema kuwa changamoto hiyo imekuwa iksababisha kusimamisha kazi kwa muda wa masaa kadhaa na wakati mwingine baadjhi ya vifaa kuungua.

“Sisi kama wateja wakubwa chanagomoto kubwa tunayoipata ni umeme unaochreza wakati shuguli za kiwanda ikiendelea hali hii inasababisha vifaa vyetu kuungua na wakati mwingine tunalazimika kusitisha shuguli za uzalishaji kwa muda, tunaomba hili lirekebishwe” alisema.

MWISHO 

Na Esther Macha,Mbozi

WAKULIMA wa vijiji vya kata ya Isansa na Magamba Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, wamelalamikia wakala wa mbegu ya Kibo Seeds kuwauzia mbegu feki ambazo hazikuota, ambapo wamelazimika kuingia gharama ya kununua mbegu nyingine na hivyo kuwasababishia hasara ya mamilioni ya shilingi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana wakulima hao ,walisema kuwa waliuziwa mbegu aina ya Kitale Haibrid 614 ambayo inazalishwa na kampuni ya mbegu ya Kibo Seeds ya nchini Kenya.

Mmoja wa wakulima hao, Elia Shipelele alisema kuwa baada ya kugundua kuwa mbegu hizo ni feki walilaziika kutafuta begu zingine na mbolea ili kuendana na msimu wa kilimo.

Hata hivyo mkulima huyo aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kufanya ukaguzi wa mbegu kabla kupeleka kwa wakulima ili kuweza kuepuka hasara.

Kwa upande wake Ofisa kilimo na mifugo wa kata ya magamba ,clemence Mamuya alikiri kuwepo kwa tatizo hilo akidai kuwa na yeye ni miongoni kwa wakulima ambao wamepata hasara hiyo.

Alisema kuwa kutokana na tatizo hili ni vema serikali ikawa na mkakati wa kuyafuatilia makapuni na mawakala wanaosambaza mbegu kwa wakulima ili kuondoa sintofahamu kwa wakulima.

Akizungumzia malalamiko hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya Meru green Care Victor Lema Kampuni ya Meru Green Care alisema suala hilo wamelisikia kutoka kwa wakulima .

Aidha Lema alisema kuwa baada ya kupata malalamiko hayo alichukua hatua kwa kwenda ofisi ya kilimo wilaya na kuamuliwa kuwasiliana na kampuni ya mbegu ya Kibo seeds ambao walitaka idadi ya majina ya wakulima waliopatwa na tatizo hilo.

Hata hivyo Lema alisema jumla ya wakulima 80 wameathirika na tatizo hilo la mbegu feki katika wilaya ya Mbozi.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...