Wednesday, 30 March 2016

JAMII IWE MAKINI NA MATANGAZO YA NAMNA HII

Na:George Binagi @BMG
Hili ni miongoni mwa Matangazo yanayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii. Awali matangazo kama haya ikiwemo lile la Kujiunga na Freemason pamoja na watalaamu wa tiba asili yalizagaa pia mitaani na hata katika mitandao ya kijamii.

Asilimia kubwa ya matangazo haya yanaonekana kuwa ya kuwalaghai wananchi kupitia shida na matatizo yao hususani katika magonjwa.

Nakumbuka mwaka jana Serikali ilipiga marufuku matangazo yote ya waganga wa kienyeji katika mabango ya mitaani, mitandao ya kijamii na hata katika vyombo muhimu vya habari kama vile redio, runinga na magazeti, kutokana na matangazo hayo kujaa upotoshaji kwa baadhi ya maeneo ikiwemo kutibu magonjwa sugu ikiwemo Ukimwi nk.

Hata hivyo katazo hilo halikuzaa matunda kama ilivyotarajiwa, kwani lilizua mvutano mkali baina ya serikali na waganga wa jadi (hupenda kuitwa watalaamu wa tiba asili), na sasa kasi ya matangazo hayo imeongezeka maradufu zaidi.

Ni kutokana na upotoshaji wa baadhi ya matangazo hayo, Binagi Blog inahoji; Ni nani mwenye jukumu la kufuatilia matangazo yanayobandikwa katika mitaa, kwenye runinga, magazeti pamoja na kwenye mitandao ya kijamii ili kuondoa athari za matangazo hayo katika jamii?.

Mfano mzuri ni tangazo hapo juu ambalo limeonekana kubandikwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Jijini Mwanza, na sasa linasambaa kwa kasi katika mitandao ya Kijamii, kwamba kuna biashara mpya ya ununuzi wa mkojo wa binadamu.

Kwa tangazo kama hili pamoja na mengineyo mengi, ni vyema viongozi wa serikali katika janja zote ikiwemo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo wakachukua hatua dhidi ya wahusika ili kuondoa upotoshaji unaojitokeza ama unaoweza kujitokeza kutokana na matangazo yenye upotoshaji katika jamii. Pia wanajamii wawe makini na matangazo ya aina hiyo.
Bonyeza HAPA Kusoma Tangazo Jingine la Upotoshaji.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...