Friday, 18 March 2016

SERIKALI YAPONGEZA OPERESHENI SAFISHA YA TFDA, WAUZA DAWA ZA SERIKALI KUHUKUMIWA


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amepongeza juhudi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nchini kwa hatua wanazochukua katika utendaji wake ikiwemo zoezi la kukagua madawa yasiyofaa kwa Jamii ikiwemo yale yaliyokwisha muda wake hasa katika zoezi la "Operesheni Safisha" iliyofanywa karibu mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara huku akitaka wale wote waliohusika kupandishwa Mahakamani kwa hatua za kushughulikiwa.

Kigwangalla ameyasema hayo mapema jana Machi 17 jijini Dar es Salaam baada ya kupewa matokeo ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na yasiokuwa na vibali iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA pamoja na Jeshi la Polisi, amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka katika hospitali za serikali.

Amesema kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.

Kigwangalla amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.

Aidha amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.

Operesheni hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685 katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za asili.

Aidha Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi

Kigwangalla amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali katika duka la dawa.

Amesema kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote waliokutwa na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa dawa hizo.

Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa



Msajili wa Baraza la Famasi nchini, Bi. Elizabeth Shekalaghe akisoma ripoti ya Operesheni Safisha kwa Naibu Waziri pamoja na wanahabari na wakuu wa idara ya TFDA (hawapo pichani). 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akitoa taarifa yake juuu ya Operesheni Safisha


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma tamko la Serikali ikiwemo juu ya kuwachukulia sheria kali wahusika wanaohujumu sekta ya Afya hasa upande wa madawa tiba ikiwemo watumishi wanaoiba dawa za Serikali pamoja na wale wanaoendesha maduka ya dawa bila kuwa na vibari.


Baadhi ya maafisa kutoka TFDA na Famasia wakifuatilia tukio hilo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa tamko hilo.


Mwanahabari wa mtandao wa Michuzi Blog, Bw. Chalila Chibuda akiuliza swali kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.


Meza kuu ikisikilia swali kwa umakini kutoka wa wanahabari (hawapo pichani).


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali ya wanahabari.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaonesha wanahabari baadhi ya vitu vilivyokamatwa katika Opresheni Safisha. kifaa alichokishika Naibu Waziri ni miongoni mwa vifaa vilivyokutwa vinatumika kuchemshia vifaa vya kufanyia upasuaji/operesheni ikiwemo vifaa vya kutolea mimba.


Baadhi ya vifaa na madawa vilivyokutwa wakati wa operesheni hiyo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla moja ya dawa ambayo ni ya usingizi hata hivyo ilikutwa katika maduka ya dawa ya kawaida


Madawa hayo.


Madawa hayo yaliyokamatwa.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa agizo la Kiserikali juu ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wahusika waliokamatwa kwa kukutwa na dawa zilizokwisha muda wake, maduka yasiyokuwa na wafamasia waliosomea na yale yenye kuendeshwa kienyeji.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...