Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akimkabidhi picha yake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard kasesela (kulia) baada ya kushinda mnadi wa ununuzi wa picha hiyo wakati harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa katika Parokia ya Kilolo jana.
Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) amefanikiwa kuchangisha zaidi Tsh mil 142 na $200 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa katika parokia ya Kilolo jana.
Askofu Ngalalekumtwa katika ‘Siku ya Mlo wa Hisani’ alitoa mchanganuo wa michango iliyopatikana katika harambee hiyo kuwa fedha taslimu zilikwa shilingi milioni 15,845,000.100 pamoja dola za kimarekani 200 na ahadi zilikuwa milioni jumla shilingi milioni 128,570,000/-.
Baba askofu Ngalalekumtwa alishukuru wadau wote na amewaomba wadau wengine wajitokeze kujenga nyumba ya Mungu ya kisasa pale Kilolo.
Aidha, askofu huyo alitoa baraka kwa wale wote waliojitolea kuchangia ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Kilolo katika Jimbo la Iringa na kuwaomba waendelee na moyo huo wakitoa kwa kuchangia maendeleo.
Katika siku hiyo ya hisani alikuwepo Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza na wakuu wa wilaya KILOLO na MUFINDI pia walishiriki katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kilolo.
Wengine waliohudhuria harambee hiyo ni pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa Alex Kimbe, wadau mbalimbali mkoani Iringa, viongozi wa serikali na siasa ilifanyika katika Ukumbi wa Kichangani mjini Iringa.
Baada ya harambee kulikwapo na kabumbu iliyochezwa katika yaa wadau na maparoko ambapo maporoko waliwabamiza wadau goli 1-0. Kikosi cha wadau kiliongozwa na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
“Tulijitahidi sana pamoja na kufanya usajili wa papo kwa papo. Maparoko walionyesha wana uzoefu na wanafanya mazoezi..., “alisema DC Kasesela.
No comments:
Post a Comment