Monday, 4 April 2016

KLSA ASSOCIATES YAJIUNGA NA PKF, PROF. ASSAD AWATAKA KUONYESHA UBORA ZAIDI




Mgeni rasmi katika halfa ya uzinduzi wa ofisi za PKF Associates, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad akiwasili ukumbini na kukabidhiwa zawadi. (Picha na Rabi Hume wa Modewjiblog)

Katika kuhakikisha wanajitanua katika utoaji wa huduma bora za uhakiki na ukaguzi wa hesabu, kampuni ya KLSA Associates ya nchini imejiunga na mtandao wa kimataifa wa makampuni ya hesabu za kifedha na ushauri ya PKF ambapo baada ya kujiunga imebadilika jina kutoka KLSA Associates na kuwa PKF Associates Tanzania.

Akizungumza katika halfa ya KLSA kujiunga PKF, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad aliwapongeza KLSA kujiunga na PKF na kuwataka kuongeza juhudi na kuboresha huduma zaidi kwa kuzingatia kwa sasa wamejiunga na kampuni ambayo inasifika duniani katika ukaguzi wa hesabu, utunzaji wa hesabu za kifedha, ufumbuzi na ushauri wa masuala ya kodi na kibiashara.

“Tunafahamu jinsi PKF wanavyofanya kazi, mmepata nafasi ya kujiunga nao na itarahisisha kwenu kupata hata taarifa nyingi hivyo ni wakati wa kuonyesha kuwa ninyi ni bora katika kutoa huduma,” alisema Prof. Assad.

Nae Meneja Mshirika wa PKF Associates Tanzania, Mustasir Gulamhussein alisema wameamua kujiunga na PKF kwa kutambua uwezo wao wa kufanya kazi katika maeneo mbalimbali duniani na wanaamini kujiunga kwao kutawawezesha kujitanua katika utoaji wa huduma bora zaidi kutokana na kuwa na wafanyakazi walio na uwezo.

“PKF ni jina linaloheshimika na kutambulika katika uhifadhi wa taarifa za kifedha ulimwenguni na kwa kuwepo Tanzania kunadhihirisha umuhimu wake katika kuwahudumia wateja ambao wanapanua wigo wao kimataifa na tunaamini tutakuwa zaidi katika kutoa huduma,” alisema Gulamhussein.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa PKF Kanda ya Afrika, Theo Veemark alisema KLSA ni kampuni nzuri katika utendaji wao wa kazi za uhakiki na ukaguzi wa hesabu hapa nchini na wanaamini kufanya kazi na KLSA kutawawezesha kutanua huduma zao zaidi na kurahisisha utendaji wa kazi.

“Tunafuraha kuwakaribisha KLSA katika familia ya PKF tunaamini kupitia muungano huu tutaweza kutanua soko letu la kibiashara na kubadilishana mawazo ili tuweze kuboresha huduma zetu zaidi,” alisema Veemark.


Meneja Mshirika wa PKF Associates Tanzania, Mustasir Gulamhussein akielezea KLSA kujiunga PKF na matarajio yao.


Mkurugenzi wa PKF Kanda ya Afrika, Theo Veemark akielezea soko la biashara na jinsi watakavyofanya kazi.



Mkurugenzi Mtendaji wa PKF kwa Afrika Mashariki, Atul Shah akielezea jinsi PKF inavyozidi kujitanua na kupata nafasi ya kuboresha huduma zaidi.


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad akitoa hutuba na kuwapongeza KLSA kujiunga PKF.



Mshereheshaji wa halfa hiyo, Taji Liundi.


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad akimkabidhi Meneja Mshirika wa PKF Associates Tanzania, Mustasir Gulamhussein cheti cha PKF kuashiria KLSA kujiunga na PKF.


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad akikabidhi mfano wa hundi ya Dola 4,000 kwa Shule mbili za Wilaya ya Mkuranga, Pwani kwa ajili ya sola ambazo zitagawiwa kwa wanafunzi.


Mkurugenzi wa PKF Kanda ya Afrika Mashariki, Murtuza Dalal akimkabidhi zawadi ya shukrani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad.


Meneja Ukaguzi wa PKF Associates Tanzania, Azim Budhwani akitoa neno la shukrani na kufunga halfa hiyo.


Waalikwa wakifurahi baada ya kumalizika kwa halfa hiyo ya KLSA kujiunga na PKF.






No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...