Washiriki mbalimbali wa mkutano wa pili wa wadau wa kidakio kidogo cha maji cha Mto Mbarali wakifuatilia mkutano unaoendelea mjini Makambako, mkoani Njombe.
Mratibu wa WWF Programu ya maji Ruaha, James Mturi akitoa utangulizi wa warsha kwa wadau kuwa Shirika la WWF Tanzania kupitia Programu ya Maji Ruaha na Ofisi za Maji Bonde la Rufiji kwa kipindi cha miaka miwili zimetekeleza mradi katika eneo bonde dogo la Mto Mbarali.
Lengo la mradi likiwa ni kuwashirikisha wadau katika upatikanaji, utumiaji na usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji za bonde dogo la Mto Mbarali, kurudisha mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu. Kupitia mradi huu wadau mbalimbali walishiriki kuibua shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji na kuzitekeleza chini ya usimamizi wa Ofisi ya maji bonde la Rufiji na Shirika la WWF.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Asumpta Mshama akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa wadau wa bonde dogo ka mto Mbarali unaofanyika Ukumbi wa Midtown, Makambako.
No comments:
Post a Comment