Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale
Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho,
Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.
Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.
Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.
“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.
Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.
Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.
Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
No comments:
Post a Comment