MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA)imevipiga faini ya milioni 5 vituo vya utangazaji vya Clouds Redio na kituo cha Independent Television (ITV ) huku pia ikipiga faini ya milioni 4 kituo cha Clouds Tv pamoja kuvipa onyo kali vituo hivyo,baada ya kukiuka kanuni za utangazaji .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akitoa hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa (TCRA)Mapunda amesema vituo vyote vimekiuka kanuni ya utangazaji ya mwaka 2005 baada ya kutenda makosa tofauti ambayo yenye lengo la kuipotosha jamii.
Mapunda amedai kuwa mnamo tarehe 9/05/2016 kituo cha Clouds Rediokatika kipindi cha Jahazi kilikiuka kanuni hizo baada ya mtangazaji wa kipindi hicho Eprahimu Kibonde kushabikia kijana mwenye umri wa miaka 14 ambaye alifanya mapenzi ya mbuzi.
Amesema katika kipindi hicho mtangazaji huyo alionekana kushabikia hali hiyo baada ya kusema Kijana aliyefanya mapenzi na mbuzi ilitakiwa atoe posa kwa mbuzi huyo, jambo ambalo linakwenda kinyume na sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 Na.5(c),5(g),14(1).
Amesema baada ya kamati yake kubaini makosa hayo waliwasilina na uongozi wa Clouds media kutaka kupata utetezi wa kosa hilo lakini mmiliki wa Clouds redio Ruge Mtahaba ambapo katika maelezo yake ya awali alikili kosa kwa watangazaji hao kutozingatia sheria hiyo huku akiomba Mamlaka hiyo kuwasamehe.
Mbali na kipindi hicho pia Kamati hiyo imebaini ukiukwaji wa sheria hiyo kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku saa 12 asubuhi hadi saa 10 asubuhi ,amedai kuwa siku ya tarehe 18/5/2016 katika redio hiyo watangazaji wa kipindi hicho walitumia maneno yasiyo na staha.
Amedai kuwa katika kipindi hicho watangazaji hao walisoma taarifa kwenye magazeti inayosema “Mtoto wa miaka mitatu apandikishwa Uume” huku watangazaji hao wakiwasilisha taarifa hiyo kwa mzaha yenye kujaa kushabikia masuala ya ngono na kushindwa kusimamia kanuni za utangazaji.
Hata hivyo,amesema katika kipindi hicho kilikuwa hakina mtaalamu wa masula ya kitabibu wenye kutoa ukweli juu ya taarifa hiyo kutoka kwenye magazeti.
Mapunda amesema baada ya Mamlaka hiyo kubaini ukiukwaji huo wa kanuni waliwasiliana na Uongozi wa Redio hiyo ambapo utetezi wake walisema watangazaji hao hawakufanya makosa kwani walitoa taarifa ilivyo kutoka kwenye magazeti.
Hata hivyo,Mapunda amesema utetezi wa Clouds Redio haukuwa na mshiko kwani watangazaji hao walishindwa kusimamia sheria ya utangazaji ya 2005 inayokataza kurusha maudhui yenye matusi kuanzia saa 11.30 alfajili hadi saa 3 usiku kwani mda huo watoto wanakuwa macho.
MAKOSA YA CLOUDS TV NA ITV.
Mapunda amesema mnamo tarehe 15/06/2016 kituo cha Independent television cha Dar es salaam(ITV) katika kipindi cha Kumekucha kilichorushwa hewani kati ya saa 1.00 asubuhi na saa 1.30 asubuhi kilitangaza uchambuzi wa Bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 ambapo mtangazaji wa kipindi hicho,Godfrey Monyo alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini,Peter Msigwa.
Amesema katika kipindi hicho Msigwa alitamka kwamba Naibu Spika Dkt Tulia Akson kuwa anavaa “Pumpers” kwa ajili ya kujisaidia kwa sababu amekuwa hawaachii watendaji wengine kiti na cha spika kwa ajili ya kuliongoza Bunge.
Mapunda amesema katika kipindi hicho mtangazaji alishindwa kuudhibiti mjadala huo jambo ambalo lilipeleka lugha za matusi kutoka.
Aidha,Mamlaka hiyo baada ya kubaini makosa hayo walifanya mawasiliano na Uongozi wa ITV,ambapo Mhariri wa kituo hicho,Steven Chuwa alitoa utetezi kuwa kipindi hicho kilikuwa live (moja kwa moja) kwahiyo ni vigumu mtangazaji kuzuia hali hiyo pamoja na hata hadhi ya Mbunge Msigwa kwenye jamii kwani yeye mwenyewe angejua aina ya maneno kutamka.
Mapunda amesema baada ya utetezi huo,Mamlaka hiyo ikabaini kituo hicho kimekuka kanuni ya utangazaji ya mwaka 2005 inayokataza kituo kutoa maauzi yenye kugombanisha umoja na mshikamano na kutoa maneno yenye kuudhi Mamlaka za serikali.
Katika hatua Nyengine TCRA imkipiga faini ya Milioni 4 kituo cha Clouds Television ambao inadaiwa mnamo tarehe 22/05/2016 katika kipindi cha “Hip Hop” kinachorushwa hewani saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni walirusha video ya “Thank for Coming” ya mwanamuziki F.A pia katika kipindi hicho walirusha wimbo wa “Lil Bebbie” unaoitwa Break it Down ambapo katika nyimbo hizi zilionyesha maudhui ya baadhi ya wanawake wanaovaa nguo za uchi.
Amedai kuwa jambo la kuonyesha video hizo ni kinyume na sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 inayokataza kuonyesha vipindi kama hivyo kwenye mda ambao watazamaji ni watoto.
Aidha,Mapunda amesema vituo vyote vilivyopewa adhabu hiyo watakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku 30 huku rufaa zikiwa wazi kwa kituo ambacho hakijalizika na hukumu hizo.
TUMECHOKA kuvumilia! Ni kauli ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai kusakamwa na Serikali ya Rais John Magufuli, anaandika Pendo Omary.
Chama hicho kimetoa kauli hiyo leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya Jaji Mstaafu, Salome Kaganda ambaye ni Kamishna wa Maadili na Mtendaji Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwaandikia barua viongozi wa chama hicho akiwatuhumu “kukiuka masharti ya Hati ya Ahadi ya Uadilifu wa Viongozi wa Umma.”
Jaji Kaganda aliwaandikia barua viongozi hao tarehe 4 mwezi huu ambapo Chadema wameitaka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuacha vitisho kwa viongozi wa chama hicho.
Walioandikiwa barua hiyo ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, kwa mujibu wa barua ya Jaji Kaganda, katika tarehe, muda na siku ambayo haijulikani, viongozi hao wa Chadema walitoa matamshi ambayo yanachochea wananchi kutotii sheria, kufanya vurugu, kudharau misingi ya demokrasia iliyopo nchini na kutishia usalama wa nchi.
“Hata hivyo, Jaji Kaganda hakuyataja matamshi hayo wala kuyafafanua. Aidha, alidai kwamba matamshi hayo yanatokana na maazimio yaliyofikiwa na kikundi cha watu wachache nje ya Bunge,” amesema Dk. Mashinji.
Licha ya kudai kwamba, maazimio ya kikundi hicho yanapuuza utangamano, utulivu na usalama wa wananchi wengine kinyume na dhana ya maslahi mapana ya umma, Jaji Kaganda hakukitaja kikundi hicho cha watu wachache nje ya bunge huku pia akidai matamshi ya viongozi hao yalilenga ‘kushamirisha ‘ maslahi yao binafsi na maslahi ya Chadema.
“Mheshimiwa Mbowe ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini. Ni kiongozi wa chama ambacho mgombea urais wake alipata zaidi ya kura milioni sita kati ya kura 15 milioni zilizopigwa kwenye uchaguzi mkuu wa urais mwaka jana.
“Ni mbunge wa kuchaguliwa na kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Katika Bunge. Ni mtu na kiongozi anayejulikana na kuheshimika ndani na nje ya Tanzania. Kusema kuwa kiongozi huyo anaongoza kikundi cha watu wachache nje ya Bunge kwenyewe ni kuonesha maadili yenye mashaka kwa mwandishi wa barua hiyo,” amesema Dk. Mashinji.
Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki ameeleza kushangazwa na barua ya Jaji Kaganda akisema;
No comments:
Post a Comment