Friday, 16 September 2016

HABARI NJEMA-WATANZANIA WALIOTEKWA KONGO TAARIFA YAKE MPYA HABARI NJEMA-WATANZANIA WALIOTEKWA KONGO TAARIFA YAKE MPYA HII HAPA



Madereva wa malori kutoka Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.


Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amezungumza na shirika la utangazaji la BBC na kusema wote wameokolewa na wako salama


Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilieleza kuwa watekaji hao ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambao baada ya kuyateka magari 8 toka Tanzania , waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Bw. Dewji. 

Waasi hao walioa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.




Kukosekana kwa fedha ya kukamilisha mchakato wa sheria ya Parole kwa wafungwa mbalimbali nchini waliomaliza nusu ya kifungo chao gerezani ni miongoni mwa sababu yakuwepo mrundakano wa wafungwa katika magereza Tanzania.


Akiongea na waandishi wa habari hii jana jijini Dar es salaam wakati akimpongeza na kisha kumteua Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa harambee ya kuchangisha fedha kwaajili ya kuwalipia wafungwa wanaotakiwa kutoka gerezani chini ya sheria ya Parole, Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Augustino Lyatonga Mrema alisema ili mfungwa atolewe gerezani ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu.


“Ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu kwenye mahakama iliyomukuhumu na waende kuonana na uongozi wa kijiji au mtaa ambapo mfungwa atenda kuishi anapotoka gerezani ikiwa ni pamoja na kuonana na familia yake na pia kuonana na watu waliowakosea ili jamii ya eneo hilo itambue kuwa ataachiwa huru” alisema


Aidha, Mrema aliwataka maofisa wa parole kote nchini kuwatembelea wafungwa waliopata Parole ili wafungwa wengi wenye sifa za kutolewa kwa sheria ya Parole wasiendelee kuteseka magerezani bali waende kuungana na familia zao sambamba na kuongeza nguvu kazi.


Kutokana na kutotengwa fedha kwaajili ya kushugulikia suala hilo, Mwenyekiti huyo wa Parole Taifa, amemteua Mama Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa kuchangisha fedha kwa kushirikisha viongozi wote wa dini nchini kushiriki harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kuwatoa wafungwa magerezani na kupunguza msongamano katika magereza nchini.


“Napendekeza kufanyike harambee kwenye makanisa yote nchini, siku ya Jumapili moja ili sadaka zote zikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani” alisema


Mrema alisisitiza kuwa wanaolengwa na Parole siyo wanye makosa ya ubakaji, mauaji, wizi kwa kutumia silaha na makosa mengine.


Naye Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare aliwataka watanzania kuangalia taifa kwanza kwani kina baba wengi wenye nguvu watarudi katika jamii na kusaidia katika uzalishaji mali sambamba na kutatua matatizo ya kiuchumi na kimaendeleo katika familia zao.


“Tutaunganisha familia zilizo sambaratika na kutaabika baada ya mzazi mmoja kufungwa miaka 6 pengine kwa kukosa faini ya milioni moja tuu, tutaondoa msongamano wa wafungwa na kulinda afya zao kutokana na magonjwa wanayopata wakiwa gerezani” alisema


Mchungaji Gutrude Lwakatare alisema anaunga mkono jitihada za bodi ya Parole Taifa na siyo kuwalinda waalifu kama ambavyo wengine watatafsiri kwani kurejesha familia ni miongoni mwa kustawisha jamii huku akinukuu maneno ya kidini yanayolenga kuwakomboa walioko kwenye vifungo na taabu mbalimbali ndani ya jamii.





Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.


Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.


Kikwete aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.


Kiongozi huyo mstaafu ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.


“Ndugu zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.


Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”


Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.





WATANZANIA 12 jana wametekwa katika eneo la Namoyo, Jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na kikundi cha waasi cha Maimai, anaandika Aisha Amran.


Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa watu hao ni madereva wa malori na kwamba, baada ya kutekwa wakiwa katika magari yao, walishushwa na kupelekwa porini na kisha malori yao manne kuteketezwa kwa moto.


Kati ya malori hayo, nane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa kitanzania, Azim Dewji na mengine ni ya wafanyabiashara kutoka Kenya.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni kwamba walipwe fedha kiasi cha Dola za kimarekani 4,000 (zaidi ya milioni Sh. Milioni 8 za Tanzania) kwa kila dereva ili waweze kuwaachia mateka hao.
“Wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha wanachokitaka itakapofika saa 10 jioni leo ingawa katika tukio hilo madereva wawili wa kitanzania, wamefanikiwa kutoroka ambao ndiyo waliosaidia kutoa taarifa rasmi,” imeeleza taarifa hiyo.
Serikali ya Tanzania imedai kuwa, tayari imechukua hatua za awali za kuwasiliana na serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa kwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama.
Hata hivyo serikali haijafafanua kuwa, ni hatua gani zimechukuliwa ili kuwaokoa madereva hao, kama ni kulipa kiasi cha fedha kinachohitajika au la.

Tukio hili ni la pili kutokea katika miaka ya hivi karibuni ambapo mwaka 2015 Mashekhe kutoka Tanzania walitekwa nchini DRC, lakini walifanikiwa kuachiwa huru bila madhara yoyote.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...