Wednesday, 19 October 2016

ZAIDI YA WADAU 100 UKANDA WA KUSINI WATASHIRIKI MAADHISHO YA UTALII


Ofisi ya mkuu wa mkoa wa iringa kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii, mradi wa kuboreha mtandao wa hifadhi zakusini mwa Tanzania (SPANEST) pamoja na na wadau mbalimbali imeazimia kufanya sherehe za maadhimisho ya utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania ujulikanao kama ‘karibu Tanzania southern circuit’.

sherehe za maadhimisho ya utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania unaojumwisha mikoa ya iringa, mbeya, katavi, songwe, morogoro na ruvuma zitafanyika kabla ya tarehe 30 November mwaka 2016 ili kwenda sambamba na maadhimisho yanayofanyika duniani kote.

Lengo kuu ya sherehe ya maadhisho hayo ni kukuza na kuendeleza utalii kikanda na taifa kwa ujumla. 

Maadhimisho ya Utalii yafanyike kwa Siku 3 kuanzia tarehe 27-29 Novemba, 2016. Tarehe hizo zimechaguliwa ili:-

-Kutoa fursa ya kutosha kwa Mkoa kufanya maandalizi ya kufanikisha sherehe hizo.

-Kutoa fursa kwa wadau wa Mikoa ya kusini kushiriki katika maandalizi na maonyesho haya ambayo yanafanyika kwa mara ya Kwanza Mkoani Iringa.

-Kwenda sambamba na kipindi cha maadhimisho ya Utalii Duniani ambacho ni kuanzia tarehe 25 Sept. -30 Nov. kila Mwaka. 

Maadhimisho hayo yatajikita zaidi katika kuutangaza Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo zaidi ya wadau 100 Ukanda wa Kusini watashiriki.Wadau hao ni pamoja na:-

-Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake (TANAPA, TAWA na TFS).

-Serikali za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Halmashauri zake.

-Wadau wa Miradi ya Maendeleo na Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira kama SPANEST, WCS, Ruaha Carnivores, STEPS, Panda Miti Kibiashara.

-Wenye Mahoteli, wasafirishaji abiria, wajasiliamali wa shughuli

na Makampuni ya Kitalii.

-Taasisi za Kifedha 

- Watoa huduma za mawasiliano kama TTCL, Tigo, Voda Com, Airtel, Zantel, Halotel na watoa huduma za ving’amuzi kama Star times, Zuku n.k.


-Taasisi za Elimu-Vyuo Vikuu vya Iringa,Mkwawa, Ruco, VETA, Chuo Kikuu Huria, na vyuo vinavyotoa

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...