Sunday, 6 November 2016

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI IRINGA CHA KUSANYA 1,218,960,000/-



Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa hotuba yake jana wakati wa kufunga maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani, kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wake RTO Leopold Fungu. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA) 






JESHI la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Iringa kimefanyiwa kukusanya 1,218,960,000/- kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani katika kipindi cha miezi tisa mwaka 2016, imeelezwa. 

Katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa ambaye pia ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa (RTO) Leopold Fungu alisema kuwa mapato hayo yameongezeka kwa asilimia 31 ikiliganisha na makusanyo ya mwaka 2015 kwa kipindi hicho hicho. 

RTO alisema kuwa mapato hayo yameongezeka hadi 1,218,960,000/- mwaka 2016 kutoka 835,800,000/- mwaka jana. 

Aidha, alisema kuwa makosa ya kawaida yameongezeka kutoka 27,787 mwaka 2015 hadi 40,632, ambapo ni sawa na aslimia 32. 

Kwa mujibu wa tathimini ya ajali za barabarani kwa kipindi cha miezi tisa mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka huu 2016 mkoa wa Iringa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani. 

Kuwa kwa kipindi cha January hadi Septemba mwaka 2015 ajali zilikuwa ni 41 ila kwa kipindi cha January 2016 hadi septemba 30 ni ajali 35 ndizo zilizotokea wakati watu waliopoteza maisha kwa kipindi cha January 2015 hadi Septemba ilikuwa ni 34 ila kwa mwaka huu toka January hadi Septemba 30 ni watu 30 ndio waliopoteza maisha. 

Aidha katika kipindi hicho ajali za piki piki zimepungua kwa asilimia 15 huku watu waliokufa kwa ajili ya pikipiki wamepungua kwa asilimia 11 na waliojeruhiwa wamepungua kwa asilimia 20 kuwa kupungua kwa matukio ya ajali ni kutokana na elimu za mara kwa mara. 

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye alikuwa mgeni rasmi aliipongeza kamati ya usalama barabara mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Salim Abri Asas kwa kuokoa maisha ya watanzania kutokana na ajali. 

Masenza alitoa pongezi hizo jana (Jumamosi) wakati wa akifunga maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo imeadhimishwa kimkoa katika viwanja vya stendi ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema mbali ya kuwepo kwa wadau mbali mbali katika kupunguza ajali na kusaidia pindi ajali zinapotokea ila serikali yake ngazi ya mkoa inatambua mchango mkubwa unaotolewa na familia ya mfanyabiashara Asas katika kusaidia kuokoa roho za watanzania pindi wanapopatwa ajali. 

“ Kana mambo mengi makubwa ambayo Asas amekuwa akijitolea kuyafanya kwa ajili ya kunusuru maisha ya majeruhi wanaopatwa na ajali ndani ya mkoa wetu, mfano katika ajali iliyotokea Changarawe mjini Mafinga kwa kuhusisha basi la Majinja ajali iliyoua watu zaidi ya 50 na kujeruhi wengine wengi …msaada mkubwa wa kuokoa roho za majeruhi kwa kujitolea dawa zilionyeshwa na Asas ….mimi nikiwa ni mkuu wa mkoa na serikali ya mkoa tunapongeza kazi nzuri ya Asas na familia yake katika kuokoa roho za majeruhi naomba Mwenyezi Mungu azidi kumuongezea pale anapopunguza kwa ajili ya wengine,” alisema mkuu wa mkoa huyo. 

Alisema kuwa wiki ya nenda kwa usalama ni kwa ajili ya kukumbushana mema yanayohusu kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuondoa vifo vinavyotokana na ajali barabarani hivyo pamoja na kumbushana kanuni na sheria za usalama barabarani ni vema kutumia maadhimisho hayo kutambua michango mbali mbali ya wadau wanaojitolea kwa jili ya kufanikisha elimu ya usalama bararani ama kusaidia kuokoa majeruhi na vinginevyo. 

“ Kumekuwepo na ongezeko kubwa la ajali za barabarani zinazohusisha pikipiki ajali hizi zinaweza kuepukika endapo waendesha na wapanda pikipiki watazingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ….natoa wito kwa wapanda pikipiki kuacha tabia ya kuendesha bila kupata mafunzo na kutokuwa na leseni suala la kuvaa kofia ngumu kwa madereva na abiria ni lazima …..acheni tabia ya kubeba abiria zaidi ya mmoja (mshikaki) …..pia kuacha kunywa pombe vikiwemo viroba wakati wa kutoa huduma ya usafiri …..kweli naumia sana kuona vijana wanakufa baada ya kuendesha pikipiki huku wakiwa wamelewa viroba”alisema mkuu huyo wa mkoa. 

Kwa watumiaji wengine wa barabara ni vema kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kufunga mikanda pindi wanapokuwa katika magari pia abiria kuacha kushabikia mwendokasi na badala yake kuwafichua madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani. 

Aidha alitaka kuanzia sasa dereva boda boda atakayebainika kusababisha ajali na kuita wenzake kwa ajili ya kumfanyia vurugu aliyesababishiwa ajali kukamatwa na washiriki wake na kufikishwa mahakamani. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri alisema kuwa kuna dhana potofu kwa baadhi ya watu kufikiri suala la usalama barabarani linahusu ajali pekee yake kwani hata kupiga honi bila sababu ama kukwamisha shughuli za barabara kwa mambo binafsi pia ni kero kwa watumiaji wengine wa barabara. 

“Tunapozungumzia sheria za usalama barabarani situ kwa ajili ya kuepusha ajali ila ni pamoja na kuepusha kero za usalama barabarani baadhi yetu tumekuwa tukifikiri usalama barabarani ni kuepusha ajali tu ila ukweli ukizingatia usalama barabarani ni pamoja na kero kubwa ya kutozingatia sheria za usalama barabarani hata kupiga honi bila sababu ni kero..., ” alisema Asasi. 

Alisema katika watumiaji wa vyombo vya moto wanaoongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabrani na kero nyingine za barabarani ni boda boda hivyo angependa kuwaomba waendesha boda boda kupunguza kero za usalama barabarani zikiwemo za kupiga honi ovyo na ajali zinazoweza kuepukika . 




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...