Sunday, 27 November 2016

Naibu waziri mambo ya ndani awapa "siri" abiria wa ubungo



Kuelekea msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi, Hamad Masauni amewataka abiria kuacha tabia ya woga na kuamua kuwafichua madereva wanavunja sheria za barabarani, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ajali zinazotokana na uzembe.

Akizungumza katika kampeni maalum ya paza sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambayo ndio nguvu kazi ya taifa.

Amesema kumekuwa na tabia ya madereva kutaka kuendesha mwendo kasi katika vipindi hivyo, hivyo maabiria wanapaswa kufahamu kuwa huko ni kuvunja sheria na wanapaswa kuwafichua.

Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakiuka sheria za usalama barabarani.

Amesema abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.

Mjumbe Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni italeta mageuzi katika kupunguza ajali.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...