Na Esta Malibiche, Iringa
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amezindua Operesheni Komaza,ambayo takribani Wanamgambo zaidi ya 200 wameshiriki katika zoezi la oparesheni komaza mkoani Iringa .
Mafunzo hayo yataenda sanjali na zoezi la kulenga shabaha ambalo litachukua siku nne porini likihusisha mazoezi ya ukakamavu pamoja na mazoezi mengine ya kijeshi kwa wanamgambo hao.
Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mlandege Manispaa ya Iringa Mkoani hapa likiwa limekusanya vijana toka vijiji vya Mboliboli, Wasa, Idodi na kwingineko wilayani Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka viongozi wote wa siasa waache mara moja kuingilia shughuli yeyote inayohusishwa na jeshi la Mgambo,na kusema kuwa jeshi la mgambo kwani jeshi halina itikadi yoyote ya kichama
.
Masenza alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea vijana uwezo wa kuwa Imara kiafya, waweze kupambana pamoja na kuwaandaa kuwa vijana wazalendo katika jamii na kwa taifa kwa ujumla.
"Jeshi la mgambo lina msaada mkubwa sana katika ulinzi wa taifa hivyo ni muhimu sote tukachukulia mafunzo haya kama chachu ya maendeleo, ulinzi na usalama hivyo," alisema Masenza
Katika kuhakikisha zoezi linaenda sawa Mkuu wa Mkoa Amina Masenza alitoa gunia la mahindi ili likasaidie chakula kwa wanamgambo wakiwa mafunzoni na akatoa shukrani kwa wadau na kusema kuwa sasa kuna uhakikia kuwa vijana hawatapata shida kwenye suala la chakula.
Awali akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliyataka makampuni ya ulinzi kuanza kutoa ajira kwa vijana waliopitia mgambo ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira mtaani.
"Tumeamua kuwa na kikosi mahili ili kisaidie kupambana na majangili pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekuwa tishio katika wilaya yetu," alisema RC.
Kwa upande wake mshauri wa mgambo wilaya ya Iringa Afande J.M Kita amewashukuru baadhi wa wadau kwa misaada waliyotoa katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Kita aliwataja baadhi ya wadau waliochangia kuwa ni pamoja na ndugu Salim Asas aliyetoa shilingi milioni moja ambayo imeziingizwa moja kwa moja katika kughalamia chakula kwaajili ya vijana hao, naye meneja wa TANROAD wilaya ya Iringa ametoa Mchele kwaajili ya vijana hao. Kisha Afande KITA akatoa rai kwa wadau ambao wataguswa kusaidia maana bado kuna uhitaji wa msaada wa hali na maali ili kufanikisha ziezi hilo.
No comments:
Post a Comment