Sunday, 6 November 2016

TANZIA: SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA


Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa Samwel Sitta amefariki dunia Hospitali Ujerumani saa 7:50 muda wa Ujerumani.

Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.

No comments:

ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchagu...