Tuesday, 6 December 2016

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO



Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.


Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. 



Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.


Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi ya Inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO), Naomi Shangani akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu mpango huo.




Na Dotto Mwaibale


BOHARI ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. 


Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.


Wateja hao ni pamoja na hosipitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hosipitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitaliza Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitaliya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete.


Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.


Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ilikuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia tasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...