Sunday, 25 December 2016

NYAMA YA NG'OMBE MJINI IRINGA YAPANDA SIKUKUU YA KRISMASI



Baadhi ya wateja wakiwa katika mmoja ya mabucha ya nyama ya ng’ombe leo mjini Iringa, mkoani Iringa wakati huu wa kusherehekea siku kuu ya Noeli. (Picha na Friday Simbaya)










IRINGA: Wakristo duniani kote wanasherehekea Sikukuu ya Krismasi, jana msongamano katika soko la Manispaa ya Iringa na mitaa maarufu ya Mashine tatu na Miyomboni iliongezeka, huku baadhi ya bidhaa zinazotumika kwenye sikukuu, ikiwemo nyama, zikiwa zimepanda bei.

Wakazi wa mjini Iringa wamesema bei ya nyama ya ng’ombe imepanda katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi.

Walisema kuwa nyama ya ng’ombe imepanda kutoka shilingi elfi sita hadi kufikia shilingi elfu sita na mia tano kwa kilo moja.

SIMBAYABLOG ilIshuhudia baadhi ya mabucha ya nyama ya ng’ombe yakiwa yamefurika wateja katika maeneo mbalimbali ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa leo asubuhi.

Elizabeth Kadaga ni mkazi wa Frelimo, Manispaa ya Iringa alisema kuwa wafanyabiashara huwa wanatumia mwanya wa siku kuu kama krismasi na mwaka mpya kuvuna faida kubwa kwa kupandisha bei ya nyama ya ng'ombe.

Alisema kuwa siku za kawaida bei ya nyama huwa ni shilingi elfu sita (6,000/-) kwa kilo, lakini katika kipindi hiki cha Noeli wafanyabiasha huwa na kawaida ya kupandisha bei ya bidhaa mbalimbali.

Aliongeza kuwa wafanyabiasha huwa na kawaida ya kuchanganya nyama na vitu vya ndani (ofals) kama vile utumbo, moyo na maini unaponunua nyama ya kawaida.

“Wauza nyama katika kipindi hiki wanakuwa na kuburi wanauza nyama wanavyotaka kuwa kujua kwamba watauza tu wanakuchanganishia na utumbo humohumo kwenye nyama ya kawaida,” alisema Elizabeth.

Naye mkazi wa kihesa katika Manispaa ya Iringa, Clementine Sambala alisema kuwa pamoja na kwamba hali ya maisha ni ngumu watu wamefurika katika mabucha kununua nyama ili kusherekea Krismasi.


Alisema krismasi ya mwaka huu imesuasua ukilinganisha na mwaka jana kila watu wanalia hali ngumu, biashara zao hazitoki na pia watu wengi hawana hela ya kununua mahitaji ya siku kuu ya krisma na mwaka mpya.

Mmoja wa wauza nyama ya ng'ombe anayeuliza nyama katika bucha iliyopo katika ya mji wa Iringa alipoongea na nipashe alisema kuwa wateja wanalifahamu hilo sio kitu kigeni.
Alisema kuwa kawaida siku kuu kama krismasi na mwaka mpya biashara huwa nzuri kwa hivyo huwa tunawachanganyia wateja nyama pamoja utumbo, na kuongeza kuwa hata siku kuu ya mwaka mpya itakuwa hivyohivyo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...