Friday, 16 December 2016

PPF WADHAMIRIA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE WAKIWEMO WANATASNIA WA FILAMU



Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Meshack Bandawe, akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara. 




Mafunzo hayo yalanza Disemba 14 na yanafikia tamati leo Disemba 16, 2016 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Musoma. Yameandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kuwajengea uwezo wadau wa filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora.




Wadau wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, wakati akiwaeleza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo


Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, akiwasilisha mada kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara


Wadau wa filamu mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Afisa Masoko PPF, Evance Baguma


Wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara wamefurahishwa na mada kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka PPF na kuonesha mwitiko mkubwa wa kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF.

Mfuko wa Pesheni wa PPF umesema umedhamiria kuhakikisha kwamba wananchi wengi walio kwenye sekta zisizo rasmi ikiwemo wajasiriamali wananufaika na mafao ya hifadhi za jamii kupitia huduma ya Wote Scheme.


Meneja wa mfuko huo Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ameyasema hayo Musoma mkoani Mara, wakati akieleza umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo mbele ya wadau wa filamu mkoani humo.


Amesema wananchi wasio kwenye sekta rasmi wakiwemo wajasiriamali wanayo fursa ya kujiunga na mfuko wa PPF na kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu, mikopo ya elimu, maendeleo pamoja na mafao ya uzeeni kwa kila mwanachama kuchangia shilingi elfu 20 kwa mwezi ambazo mwanachama hulipa kadri awezavyo.


Naye Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, amesema lengo la mfuko huo kuanzisha huduma ya Wote Scheme kwa wajasiriamali ni kuondoa dhama potofu kwa baadhi ya wananchi kwamba anayeweza kunufaika na huduma za mifuko ya hifadhi za jamii ni lazima awe mtumishi wa taasisi binafsi ama serikali.


Wadau wengi wa filamu mkoani Mara wamefurahishwa na ufafanuzi wa mfuko huo ambapo wamebainisha kwamba awali walikosa fursa mbalimbali za mifuko ya hifadhi za jamii ikiwemo PPF kutokana ufahamu duni waliokuwa nao.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...