Friday, 23 December 2016

SHULE YA AZIMIO MANISPAA YA IRINGA YAANZA KUKARABATIWA MIUNDOMBINU YAKE











Na Friday Simbaya, Iringa

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza ukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo katika Kata ya Mshindo Manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo hayo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo Mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo kuwa miundombinu mibovu kama hiii.

Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wananfunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudunisha elimu ya wanafunzi hao.

“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa Manispaa ya Iringa halafu ikawa katika muundo huu,”alisema Kabati.

Aidha Kabati alisema kuwa ukarabati umeanza siku ya ijumaa ya tarehe 23.12.2016 na atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo Manispaa ya Iringa.

“Tuna shule bora hapa Manispaa ya Iringa, lakini hii ya Shule ya Msinggi Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa Iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu,”alisema Kabati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema haiwezekani Shule ya Azimio ikawa katika mazingira mabovu ya miundombinu kama yale hiyo hadi kufikia siku ya ijumaa atahakikisha wanaanza ukarabati shule hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Azimio, Wilfred Chotipembe alimshukuru Mbunge wa Viti Maalum Ritta Kabati, Mkuu wa Wilaya pamoja na wadau mbalimbali kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...